Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mzee wangu Azzan Zungu anazeeka vibaya, kwani hawezi kuwasilisha hoja yake bila kuwabagua watu? Kwa takwimu gani alizonazo kuweza kuwatofautisha watu waliopo mtandaoni! Nimkumbushe kina Sarungi, Karume, 2014 na wengineo wengi sio wakazi wa huko alipopataja.
Azzan Zungu: Najua hawa wote wanaoponda ponda kwenye mitandao hawakai Ilala, wao wanakaa Kivule, Bombambili, Majimatitu. Sisi watu wa Ilala tunataka maendeleo.
Tunataka lami kwenye majimbo ya Mjini tuweze kuchangia pesa za kutosha tusaidie majimbo ambayo hayana uwezo, leo Ilala tunakusanya bilioni 1.1 kwenye ada ya kupaki magari tu kwa mwezi.