Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,933
- 988
Mkazi mmoja wa Arusha alimuaga mkewe anakwenda Dar kwa safari za kikazi. Kumbe safari ikawa ni kwenda Loliondo kwa babu.
Mkewe naye, akaona huu ndiyo wakati haswa wa kwenda kwa babu. Akalianzisha.
Huko Semunge, kila mmoja kwa wakati wake akiwa anasubiri kikombe cha babu njaa ilimuuma. Mzee kumbe alikwenda na "kipoozeo". Akiwa maeneo ya mabanda akamtaka kipozeo akanunue chakula ilihali yeye akipumzika chini ya mti. Kipoozeo akaenda.
Hamadi, mkewe akamfuma hapo kwenye mti na kuanza kuzozana.
Kipoozeo asijue kitu, akaja na chakula. Lol, kamkuta mzee anazozana na mkewe. Wamefumwa huko.
Source: Radio WAPO,Kipindi cha YALIYOTOKEA,31/3/2011
Nini kilitokea juu kipoozeo na mke, hawakueleza.
My take: Ilichorwa na Masoud Kipanya, sasa imetokea kweli.