[B]Hatimaye imekuwa...Wamefumaniana Loliondo[/B]

[B]Hatimaye imekuwa...Wamefumaniana Loliondo[/B]

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
1,933
Reaction score
988
Mkazi mmoja wa Arusha alimuaga mkewe anakwenda Dar kwa safari za kikazi. Kumbe safari ikawa ni kwenda Loliondo kwa babu.
Mkewe naye, akaona huu ndiyo wakati haswa wa kwenda kwa babu. Akalianzisha.
Huko Semunge, kila mmoja kwa wakati wake akiwa anasubiri kikombe cha babu njaa ilimuuma. Mzee kumbe alikwenda na "kipoozeo". Akiwa maeneo ya mabanda akamtaka kipozeo akanunue chakula ilihali yeye akipumzika chini ya mti. Kipoozeo akaenda.
Hamadi, mkewe akamfuma hapo kwenye mti na kuanza kuzozana.
Kipoozeo asijue kitu, akaja na chakula. Lol, kamkuta mzee anazozana na mkewe. Wamefumwa huko.

Source: Radio WAPO,Kipindi cha YALIYOTOKEA,31/3/2011

Nini kilitokea juu kipoozeo na mke, hawakueleza.

My take: Ilichorwa na Masoud Kipanya, sasa imetokea kweli.
 
Hadithi hii inatufundisha tuache uongo kwa wake na waumme zetu.
 
Hiii senema ya loliondo ishaanza kunichosha..........
 
Mi sitaki kuamini, kwani huko kwa babu ni kutalii? mbona babu alisema dhmbi mwiko, bila hivyo huponi. Na hao wana ndoa wanafichana magonjwa? mambo mengine bwana uwongo umezidi.
 
Hadithi hii inatufundisha tuache uongo kwa wake na waumme zetu.

Hii si hadith ni kisa. Si kitu cha kutunga ni habari halisi.
Ila kuhusu fundisho, nakubali kuwa ni ya mafundisho tunayoweza pata.
 
Mie ndo hapo napochoka unaishije na mtu ndani halafu mnafichana mambo??? Wameumbuka sasa
 
safi lakini wajifunze kuaminiana:smile-big:
 
Back
Top Bottom