B.K inahesabika ni miaka kadhaa ukirejea baada ya Kristo, K.K ni miaka kadhaa kabla ya kuzaliwa Kristo tangu lini.?

FAJES

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2017
Posts
720
Reaction score
644
Wanabodi, naweza kuonekana kama mtu niliye na ufahamu mdogo kwa kukosa uelewa wa jambo dogo sana kama hili.

Lakini, ni swali ambalo sijafanikiwa kupata majibu kwa kipindi kirefu sasa, maana nilimezeshwa tu tangia huko darasa la ukwanza (Primary). Nimejaribu pia ku-google ila sijafanikiwa kupata jibu murua.

Inaeleweka vema kuwa, tunaposema labda 20BK maana yake ni miaka 20 baada ya Kristo kuzaliwa. Sasa tunaposema 20KK ni miaka 20 Kabla ya Kristo kuanzia lini.? Tangu kuumbwa kwa ulimwengu ama.? Na je, mwaka wa mwisho ulikuwa mwaka upi na ndipo ikwa mwaka 0 (sufuri) na kisha tukaanza mwaka 1 yaani 1BK.?

Wajuvi wa mambo haya tafadharini naomba mniondolee tongotongo katika hili jambo ili nami niwe sawa kama mlivyo ninyi juu ya jambo hili.

Wasalaam,
FAJES.
 
20kk maana yake ni urudi nyuma miaka 20 kabla Yesu kuzaliwa.
Tunaposema leo ni 2018, tunahesabu kuanzia mwaka aliozaliwa Yesu, au Yesu alizaliwa miaka 2018 iliyopita.
Kwa hiyo unaposema 20kk, unamaanisha kuwa miaka ishirini nyuma kabla ya kuanza kuhesabu mwaka aliozaliwa Yesu.
 
Mkuu nashukuru kwa udadavuzi, sasa inamana ni kuhesabu miaka kadhaa nyuma tangu kuzaliwa mpaka lini huko nyuma.?
 
Halafu hatuna B.K tuna B. C tukisema KK ni Kiswahili
 
Mkuu nashukuru kwa udadavuzi, sasa inamana ni kuhesabu miaka kadhaa nyuma tangu kuzaliwa mpaka lini huko nyuma.?
Hiyo idadi ya miaka kurudi nyuma ndio sijui, miaka ya kale watu walihesabu kwa kufuata matukio yaliyotikisa dunia.
Mfano Wakristo huhesabu kuanzia Adam na Hawa kuumbwa, Safina ya Nuhu, Sodoma na Gomora kuchomwa moto na kuzaliwa kwa Yesu.
Na husemekana kuwa interval ya tukio na tukio inasadikika ni miaka 2000, hivyo wana Thiolojia wengi wanadai tangu Adam hadi sasa ni zaidi ya miaka 6,000.
Nina kitabu cha historia cha Hebrew nitakipitia upya
 
Nashuku

Nashukuru sana Mkuu. Inaonesha dhahiri pia kuwa, maisha ya huko nyuma kabla ya Kristo ni marefu sana ukilinganisha na maisha baada ya YESU kuzaliwa. Ukipitia hicho kitabu usisite kuongezea nondo hapa..

Chakushangaza ni kuwa, Archeaologists kuna baadhi ya matukio katika BIBLIA wanafanana juu ya utafiti wao na yale yaliyomo katika BIBLIA. Kwa mfano, uwepo wa kabila la WAHITI, kuhusu kuanguka kwa ukuta wa YERIKO, uwepo wa vibao vilivyoonesha Sheria za Mungu kupitia Musa n.k, lakini juu ya historia ya miaka Wanahistoria wanatofautiana kwa kiasi kikubwa na BIBLIA, maana wao wanasema Dunia imekuwepo takribani miaka milioni kadhaa huko nyuma...
 
Mkuu hata wana Thiolojia pia wamepishana mawazo.
Mfano mzuri ni kitabu cha Ayubu, hiyo Nchi ya Usi alikoishi Ayubu, wengine wanasema aliishi dunia kabla ya Adam, yaani kuna maisha ya watu kabla ya Adamu, kuwa Mungu aliugharikisha huo ulimwengu akaanza upya, ktk hili wamekosa kujua kwa usahihi ni nyakati zipi aliishi.
Historia ya kale ni suala gumu kidogo na kila mtu amejenga hoja ktk matukio flani flani
 
1522055407262%7E2.jpeg
 
Mkuu umedodosa HOJA nzito sana..Naweza kupata references ya hoja hii nikajisomea...??
 
Tafuta kitabu kinaitwa THE WILL OF ZEUS kina taarifa myingi sana za kihistoria.
 
Nashuku

Nashukuru sana Mkuu. Inaonesha dhahiri pia kuwa, maisha ya huko nyuma kabla ya Kristo ni marefu sana ukilinganisha na maisha baada ya YESU kuzaliwa. Ukipitia hicho kitabu usisite kuongezea nondo hapa..

Chakushangaza ni kuwa, Archeaologists kuna baadhi ya matukio katika BIBLIA wanafanana juu ya utafiti wao na yale yaliyomo katika BIBLIA. Kwa mfano, uwepo wa kabila la WAHITI, kuhusu kuanguka kwa ukuta wa YERIKO, uwepo wa vibao vilivyoonesha Sheria za Mungu kupitia Musa n.k, lakini juu ya historia ya miaka Wanahistoria wanatofautiana kwa kiasi kikubwa na BIBLIA, maana wao wanasema Dunia imekuwepo takribani miaka milioni kadhaa huko nyuma...
Mkuu, Biblia sio kitabu cha historia ingawa kina historia ambayo mara nyingine Wana historia wanakubaliana nayo. Hivyo, usitumie Biblia kuthibitisha ukweli wa Archeologists au kuwakanusha wanasayansi wengine. Archeology inahesabu miaka tofauti kabisa na Biblia, Archeologists wanasema binadamu alipitia hatua kadhaa miaka milioni kadhaa iliyopita kutoka nyani/sokwe hadi kuonekana kama alivyo leo wakati Biblia inasema mwanadamu aliumbwa akiwa mtu kamili kama anavyoonekana leo na kuwa kutoka uumbaji hadi leo haijafika hata miaka elfu 10.

Biblia ni kitabu cha kiimani wakati wanasayansi wanataka facts ingawa hiyo ya evolution kutoka kuwa homosapiens hadi kuwa mtu haina facts zozote.

Vv
 
Back
Top Bottom