B.K inahesabika ni miaka kadhaa ukirejea baada ya Kristo, K.K ni miaka kadhaa kabla ya kuzaliwa Kristo tangu lini.?

B.K inahesabika ni miaka kadhaa ukirejea baada ya Kristo, K.K ni miaka kadhaa kabla ya kuzaliwa Kristo tangu lini.?

Zawad ya pasaka
FB_IMG_1522064156098.jpg
 
Mkuu, Biblia sio kitabu cha historia ingawa kina historia ambayo mara nyingine Wana historia wanakubaliana nayo. Hivyo, usitumie Biblia kuthibitisha ukweli wa Archeologists au kuwakanusha wanasayansi wengine. Archeology inahesabu miaka tofauti kabisa na Biblia, Archeologists wanasema binadamu alipitia hatua kadhaa miaka milioni kadhaa iliyopita kutoka nyani/sokwe hadi kuonekana kama alivyo leo wakati Biblia inasema mwanadamu aliumbwa akiwa mtu kamili kama anavyoonekana leo na kuwa kutoka uumbaji hadi leo haijafika hata miaka elfu 10.

Biblia ni kitabu cha kiimani wakati wanasayansi wanataka facts ingawa hiyo ya evolution kutoka kuwa homosapiens hadi kuwa mtu haina facts zozote.

Vv
Mkuu, nashukuru kwa maelezo yako fikirishi na kinzani kwa upande flani. Pamoja na utofauti huo, ni mawazo yangu kuwa, baada ya kujifunza kutoka katika references mbalimbali (i.e Archeaological and Biblical), ni kazi ya msomaji kukaa chini na kuuchambua ukweli yeye mwenyewe.

Kutokana na kutofautiana kwa kiwango cha Imani baina ya mtu na mtu, ni sahihi pia nikihitimisha kwa kusema kuwa, historia kutokana na BIBLIA ndiyo main reference to consider kutokana na kiwango changu cha imani. Hali kadhalika, hoja hii inaweza kuwa haina uzito na maana kubwa kwa mtu mwingine kulingana na kiwango chake cha imani. Hivyo, katika hoja hii kwa upande wangu nadhani kuwa, imani ya mtu ni " main driving factor' ya argument zake.
 
Mkuu, nashukuru kwa maelezo yako fikirishi na kinzani kwa upande flani. Pamoja na utofauti huo, ni mawazo yangu kuwa, baada ya kujifunza kutoka katika references mbalimbali (i.e Archeaological and Biblical), ni kazi ya msomaji kukaa chini na kuuchambua ukweli yeye mwenyewe. Kutokana na kiwango cha imani ya mtu na mtu kutofautiana, ni sahihi pia nikihitimisha kwa kusema kuwa, historia kutokana na BIBLIA ndiyo main reference to consider kutokana na kiwango changu cha imani. Hali kadhalika, hoja hii inaweza kuwa haina uzito na maana kubwa kwa mtu mwingine kulingana na kiwango chake cha imani. Hivyo, katika hoja hii kwa upande wangu nadhani kuwa, imani ya mtu ni " main driving factor' ya argument zake.
Sahihi kabisa, mkuu.

Vv
 
Back
Top Bottom