Baaada ya beki Banda wa Mtibwa Sugar FC kuhongwa ili ajivunje, sasa ni zamu za akina Yondan na Nyosso wa Geita Gold FC nao kuhongwa wajivunje

Baaada ya beki Banda wa Mtibwa Sugar FC kuhongwa ili ajivunje, sasa ni zamu za akina Yondan na Nyosso wa Geita Gold FC nao kuhongwa wajivunje

NASHINDWA KABISA KUELEWA MODS WA HILI JUKWAA WANAFANYA KAZI GANI KAMA MTU ANAWEZA KUANZISHA MADA NA KUTOA TUHUMA NZITO BILA HATA KUWEZA KUYATHIBITISHA NA BADO AKAACHWA TU NA TUHUMA ZAKE ZIKABAKI KUELEA HUMU.

HII INAONYESHA PICHA MBAYA SANA NA INAFANYA WATU MAKINI KUKOSA IMANI NA HILI JUKWAA.

PLEASE MODS WAKE UP AND HAVE THE AUTHOR ACCOUNT FOR HIS ALLEGATIONS OTHERWISE SLAP A DETERRENT BAN ON HIM/HER TO SAVE THE FORUM FROM LOSING CREDIBILITY IT IS RENOWNED FOR.
 
Tuhuma nzito kama hizi ni vyema uende uka ziripoti PCCB.

Unless otherwise zitaendelea kukutesa kwenye moyo wako na mwishowe utapata sonono na ndugu zako wakipoteza.

Sitachoka kukuambia ndugu @Maghtier kua akili zako zinatakiwa zikue sasa.
 
NASHINDWA KABISA KUELEWA MODS WA HILI JUKWAA WANAFANYA KAZI GANI KAMA MTU ANAWEZA KUANZISHA MADA NA KUTOA TUHUMA NZITO BILA HATA KUWEZA KUYATHIBITISHA NA BADO AKAACHWA TU NA TUHUMA ZAKE ZIKABAKI KUELEA HUMU.

HII INAONYESHA PICHA MBAYA SANA NA INAFANYA WATU MAKINI KUKOSA IMANI NA HILI JUKWAA.

PLEASE MODS WAKE UP AND HAVE THE AUTHOR ACCOUNT FOR HIS ALLEGATIONS OTHERWISE SLAP A DETERRENT BAN ON HIM/HER TO SAVE THE FORUM FROM LOSING CREDIBILITY IT IS RENOWNED FOR.
Bahati nzuri hawana Upumbavu kama uliobarikiwa nao na ambao pia Utakufa nao na utaishi nao Milele huko Udongoni ambako Utafukiwa.
 
Kwa nini ukate kiuno wakati anayeshughulikiwa ni mwingine , mtoa mada una ngenye za fisimaji.
 
Ukiujua Mpira wa Bongo (Tanzania) na Janja Janja yake ni raha sana.

Pongezi sana Kocha wa Mtibwa Sugar FC Salum Mayanga kwa Kuwaanzisha Wachezaji wabovu ila baada ya Yanga SC kufunga Goli la Pili ndipo ukawaingiza Wachezaji wazuri akina Kibaya.

Hongera sana Kipa Shabaan Kado (mwana Yanga SC lia lia) na Beki Abdi Banda (mwana Simba SC ila mwenye Bifu na Simba SC kwakuwa ilikataa Kukusajili tena) kwa Kukunja Pesa za Matajiri wa Avic Town na Kusambaza kwa Wachezaji kadhaa ili mfungwe na Pengo liwe ni Alama (Points) nane (8)

Hongera nyingi sana pia kwa Kiungo Mpumbavu wa Mtibwa Sugar FC ambaye ulipewa Pasi nzuri ila kwa Makusudi yako na baada ya Muamala wako Kukamilika ukaamua Kulazimisha kutaka kumpiga Chenga Feisal Salum na Kujikosesha kwa Makusudi na akaunasa na Goli Kufungwa kisha Mechi ilipomalizika ukawa Unatabasamu hata hukuumia.

Mwisho kabisa nitoe Pongezi kwa Beki Ibrahim Ame (ambaye Jana ndiyo ulikuwa Nahodha) kwa Kitendo chako cha ulipoumia ulitakiwa Kutolewa nje aingie mwingine na ukakataa ukisema unaweza kuendelea kwani hukuumia mno ila baada ya Fiston Mayele Kufunga Goli la Pili ukaomba kutoka / Kutolewa.

Beki Abdi Banda Hela ulizopewa na Matapeli wa Avic Town ni nyingi ili tu Udanganye (Ujivunje) usicheze Mechi ya jana ( huku Mratibu Mkuu wa Kukupenyezea huo Mlungula) akiwa ni Shemeji yako (Umemuolea Dada yake) Mwanamuziki Ali Kiba (mwana Yanga SC Kindakindaki) hivyo basi nakuomba zitumie katika Kuimalizia Nyumba yako ya kule Kwetu Mkoani Tanga na zingine (Chenji ) hakikisha unamalizia Kupiga Rangi Nyumba yako ya Segerea kwani Rangi iliyoko sasa inabanduka tu na Mabati nayo yanawapigia mno Kelele Majirani kwani yamelegea yanataka Kung'oka na kwa hii Mvua Kubwa ya Dar es Salaam na huu Upepo mkali yanaweza yakaanza Safari yake ndani ya Maji ya Mto Msimbazi na ukaja Kuyaokotea Baharini usawa wa lilipo Daraja liisilo na Faida kwa Watanzania na Wana Dar es Salaam la Tanzanite.

Haya Mabeki Bandidu, Masela na Wahuni mnaoogopeka na Yanga SC akina Kelvin Yondan na Juma Nyosso (ambao mna Mechi Mbili mfululizo na Yanga SC ) ile ya Ligi (NBC) na ya FA (ASFC) nanyi jiandaeni sasa Kufuatwa Kuhongwa Mamilioni na Matapeli wa Avic Town ili ama mtafute Kadi Nyekundu ili mkose Mechi nao au mkikaribia tu Kucheza nao mjivunje (mdanganye) kuwa mnaumwa au mna Dharula (kama alivyofanya Jana Beki Mpumbavu Abdi Banda) ili msicheze na Watu Washinde ili azma yao Kuu ya kwamba kwa Msimu huu / mwaka huu iwe isiwe (kwa vyovyote na gharama yoyote ) lazima wawe Mabingwa itimie.

Namalizia kwa Kusisitiza tena kuwa ukiujua Mpira wa Tanzania (Bongo ) na Umafia wake (Janja Janja yake ) ni raha sana na wala ukisikia / ukiyasikia Matokeo fulani hupati taabu sana sana utabaki Kucheka tu na Kuusikitikia ( Kuuonea Huruma ) Mpira wa Tanzania ambao una 95% ya Rushwa ( Match Fixing ) ila TFF, BMT na TAKUKURU wananyamaza na Kuona ni Jambo lenye Afya kwa Afya ya Maendeleo ya Soka letu nchini.
Nashukuru kwa uchambuzi wako,kesho kwenye mkeka namuua mtibwa
 
Utopolo huu ujinga wao wa kununua mechi ndo maana kimataifa hamtoboi..mnatolewa round ya kwanza tu. OUT!🚮🚮🚮
 
nilikula ban ya siku 7 baada ya kusema UKWELI kwamba hii ID ni backup ya ID fulani, Ukiangalia contents ni zilezile, uandishi uleule, tone ya mwamdishi ni ileile, makapi ni yaleyale... anyways Mods sijui hua wanajionaje yaani...
 
Nikimheshimu mtu huwa nashindwa kabisa kumvunjia heshima hata akiharibu na wakati mwingine nawaachia wengine washughulike naye. Lakini kwa tabia hii ambayo kila mechi ya watani zako lazima uje utuhumu kuhongwà au kuhujumu bila ushahidi si jambo zuri. Juzi Simba kashinda na hata baadhi ya magoli mtu asiye mwanasoka angeweza kuyatilia shaka kama lile la Back pass ya Mangalu, lakini wenye damu ya soka wanajua Soka ni mchezo wa makosa ni lazima yatokee. Lakini nyie kila siku hasa wewe na Mightier na kapuuzi kengine kameibuka kanaiga uandishi wako sijui kanaitwa kaKENGE nako ovyo tu. Kwenye kikosi cha Biashara alikuwemo mchezaji mwandamizi wa Simba miaka michache iliyopita Redondo, kwa hiyo tuseme miamala ilipitia kwake? Hatuwezi kuwa Great thinkers kwa kuzushazusha mambo huku tukijiona Pure talented. Ni talent gani hii ya kuzusha mambo ambayo kesho viongozi wa timu wasio na subira wanaweza kukuamini na kupelekea kutoa adhabu kwa mchezaji na hivyo kumwaribia maisha yake. Umesahau mashabiki wa Pamba walivyokwenda kuharibu nyumba ya Juma Mhina na hata kaburi la mama yake kwa sababu ya tuhuma kama hizi Pamba ilipofungwa na Malindi na kukosa ubingwa wa Muungano? Juzi Miongoni mwa Magolikipa bora kabisa kuwa kutoa Tanzania Mohamed Mwameja(Tanzania One halisi) alieleza jinsi alivyonusurika kuuawa na mashabiki wa Simba kisa tu shabiki mmoja kasema Mwameja, Masatu na Masha wameonekana ofisini kwa Azim Dewji wakichukua fedha ili wauze mechi na Stella Artois kuepusha Dewji kuwanunulia Canter wachezaji wote wa Simba kama wangechukua kombe uwanja wa Taifa mbele ya Rais Alli Hassani Mwinyi mwaka 1993?
Uchezaji ni ajira ya vijana hawa mnaowazulia usaliti kila siku, lakini kwa vile nyie hakuna mnachogharimia mnaona sawa tu kuropoka lakini wenzenu wanaumia. Nani anaweza kuvumilia kumlipa mchezaji anayeuza mechi? Hata tuhuma zile za Mwanza zilisababisha Juma Mhina kukosa kabisa nafasi timu ya Taifa wakati alisitahili. Mwaka juzi Metacha Mnata akaingizwa kwenye Kashfa ya usaliti mechi ya Yanga dhidi ya Coast Union na mpaka Leo timu kubwa ikitaka kumsajiri kama ilivyokuwa kwa Simba dirisha dogo maneno yanazuka kuhusu uuzaji mechi timu zinaghairi.
Kama hatuna ushahidi tukae kimya. Allegations zisizoweza kuthibitika zinaharibia watu image wakati ile ni ajira kwao. Kama una tuhuma wapigie TAKUKURU moja kwa moja ili kama hazina ukweli zisimchafue mchezaji kuliko hii tabia ya ovyo ambayo Mods nao wanaiacha tu iote mizizi.
 
Back
Top Bottom