Baaada ya beki Banda wa Mtibwa Sugar FC kuhongwa ili ajivunje, sasa ni zamu za akina Yondan na Nyosso wa Geita Gold FC nao kuhongwa wajivunje

TFF waanze kufungia mashabiki sasa, Popoma anatema shudu sana
 
NASHINDWA KABISA KUELEWA MODS WA HILI JUKWAA WANAFANYA KAZI GANI KAMA MTU ANAWEZA KUANZISHA MADA NA KUTOA TUHUMA NZITO BILA HATA KUWEZA KUYATHIBITISHA NA BADO AKAACHWA TU NA TUHUMA ZAKE ZIKABAKI KUELEA HUMU.

HII INAONYESHA PICHA MBAYA SANA NA INAFANYA WATU MAKINI KUKOSA IMANI NA HILI JUKWAA.

PLEASE MODS WAKE UP AND HAVE THE AUTHOR ACCOUNT FOR HIS ALLEGATIONS OTHERWISE SLAP A DETERRENT BAN ON HIM/HER TO SAVE THE FORUM FROM LOSING CREDIBILITY IT IS RENOWNED FOR.
 
Tuhuma nzito kama hizi ni vyema uende uka ziripoti PCCB.

Unless otherwise zitaendelea kukutesa kwenye moyo wako na mwishowe utapata sonono na ndugu zako wakipoteza.

Sitachoka kukuambia ndugu @Maghtier kua akili zako zinatakiwa zikue sasa.
 
Bahati nzuri hawana Upumbavu kama uliobarikiwa nao na ambao pia Utakufa nao na utaishi nao Milele huko Udongoni ambako Utafukiwa.
 
Kwa nini ukate kiuno wakati anayeshughulikiwa ni mwingine , mtoa mada una ngenye za fisimaji.
 
Nashukuru kwa uchambuzi wako,kesho kwenye mkeka namuua mtibwa
 
Utopolo huu ujinga wao wa kununua mechi ndo maana kimataifa hamtoboi..mnatolewa round ya kwanza tu. OUT!🚮🚮🚮
 
nilikula ban ya siku 7 baada ya kusema UKWELI kwamba hii ID ni backup ya ID fulani, Ukiangalia contents ni zilezile, uandishi uleule, tone ya mwamdishi ni ileile, makapi ni yaleyale... anyways Mods sijui hua wanajionaje yaani...
 
Nikimheshimu mtu huwa nashindwa kabisa kumvunjia heshima hata akiharibu na wakati mwingine nawaachia wengine washughulike naye. Lakini kwa tabia hii ambayo kila mechi ya watani zako lazima uje utuhumu kuhongwà au kuhujumu bila ushahidi si jambo zuri. Juzi Simba kashinda na hata baadhi ya magoli mtu asiye mwanasoka angeweza kuyatilia shaka kama lile la Back pass ya Mangalu, lakini wenye damu ya soka wanajua Soka ni mchezo wa makosa ni lazima yatokee. Lakini nyie kila siku hasa wewe na Mightier na kapuuzi kengine kameibuka kanaiga uandishi wako sijui kanaitwa kaKENGE nako ovyo tu. Kwenye kikosi cha Biashara alikuwemo mchezaji mwandamizi wa Simba miaka michache iliyopita Redondo, kwa hiyo tuseme miamala ilipitia kwake? Hatuwezi kuwa Great thinkers kwa kuzushazusha mambo huku tukijiona Pure talented. Ni talent gani hii ya kuzusha mambo ambayo kesho viongozi wa timu wasio na subira wanaweza kukuamini na kupelekea kutoa adhabu kwa mchezaji na hivyo kumwaribia maisha yake. Umesahau mashabiki wa Pamba walivyokwenda kuharibu nyumba ya Juma Mhina na hata kaburi la mama yake kwa sababu ya tuhuma kama hizi Pamba ilipofungwa na Malindi na kukosa ubingwa wa Muungano? Juzi Miongoni mwa Magolikipa bora kabisa kuwa kutoa Tanzania Mohamed Mwameja(Tanzania One halisi) alieleza jinsi alivyonusurika kuuawa na mashabiki wa Simba kisa tu shabiki mmoja kasema Mwameja, Masatu na Masha wameonekana ofisini kwa Azim Dewji wakichukua fedha ili wauze mechi na Stella Artois kuepusha Dewji kuwanunulia Canter wachezaji wote wa Simba kama wangechukua kombe uwanja wa Taifa mbele ya Rais Alli Hassani Mwinyi mwaka 1993?
Uchezaji ni ajira ya vijana hawa mnaowazulia usaliti kila siku, lakini kwa vile nyie hakuna mnachogharimia mnaona sawa tu kuropoka lakini wenzenu wanaumia. Nani anaweza kuvumilia kumlipa mchezaji anayeuza mechi? Hata tuhuma zile za Mwanza zilisababisha Juma Mhina kukosa kabisa nafasi timu ya Taifa wakati alisitahili. Mwaka juzi Metacha Mnata akaingizwa kwenye Kashfa ya usaliti mechi ya Yanga dhidi ya Coast Union na mpaka Leo timu kubwa ikitaka kumsajiri kama ilivyokuwa kwa Simba dirisha dogo maneno yanazuka kuhusu uuzaji mechi timu zinaghairi.
Kama hatuna ushahidi tukae kimya. Allegations zisizoweza kuthibitika zinaharibia watu image wakati ile ni ajira kwao. Kama una tuhuma wapigie TAKUKURU moja kwa moja ili kama hazina ukweli zisimchafue mchezaji kuliko hii tabia ya ovyo ambayo Mods nao wanaiacha tu iote mizizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…