Baada wa Watendaji wa Serikali za Mitaa Kawe 'Kutimka Mbio' Kuogopa 'Chatu' aliyeko katika pori la Chuo cha Tiba Lugalo msaada unahitajika

Baada wa Watendaji wa Serikali za Mitaa Kawe 'Kutimka Mbio' Kuogopa 'Chatu' aliyeko katika pori la Chuo cha Tiba Lugalo msaada unahitajika

Nina 'Style' yangu ya Uandishi na Uwasilishaji wake Wewe inakuuma nini? Kama huvutiwi nao huwa unahangaika nini Kusoma hadi Kujibu 'threads' zangu hapa JamiiForums?

Hujaanza 'Kuwashwawashwa' nami leo na inaonekana kuna unalolitafuta Kwangu hivyo endelea tu na utalipata sawa? Hujajaa vizuri katika 'Frame' nasubiri ujae ili nikupe 'Kitu' cha Kukufanya si tu Ukasirike bali Unichukie na Uichukie Milele hii ID yangu.

Nakustahi kwa Upako wa Ibada ya Jana.
Unapokuwa mgeni nchi za watu jitahidi kuwaheshimu wenyeji POPOMA wewe, mbona watz wakifika kigali na bujumbura wanakuwa na heshima?
 
Taarifa ambazo GENTAMYCINE nimethibitishiwa na Mamlaka ya Ofisi za Serikali ya Mitaa Kawe na Mtendaji Mwandamizi kutoka Jeshini Kambini Lugalo kilipo Chuo chao cha Tiba cha MCMS ni kwamba kuna uwepo wa Chatu mkubwa kiasi cha Kutishia Maisha ya Watu.

Kwa takribani Siku Tatu zimepita Wakazi wa Kawe ( hasa eneo yalipo Makaburi ) zamani kulikuwa ni Hostel na sasa Jeshi ( JWTZ ) limejenga Chuo chake cha Tiba Mamlaka ya Serikali ya Mitaa Kawe imekuwa ikipita Kuwatangazia Watu kuchukua Tahadhari ( hasa kwa Watoto ) na Watu waliokuwa na Mazoea ya Kukatisha huko Makaburini ( zamani Hostel ) kuelekea Coca Cola na Mwenge kutopita tena hiyo njia ili wasije kufanywa 'Kitoweo' Kitamu cha Chatu huyo.

Baada ya kupata Taarifa hii GENTAMYCINE niliamua kutembelea eneo la Makazi ya Watu ambapo nilibahatika Kukutana na Vijana Wawili ambao hupenda kupita hiyo njia ambao walinithibitishia kuwa ni Kweli Chatu huyo yupo na ni Mkubwa sana ambapo mara nyingi hupenda Kukaa juu ya Makaburi yaliyopo hapo.

Kumekuwa na Taarifa mbalimbali juu ya uwepo ( ujio ) wa huyo Chatu hapo ambapo wapo wanaosema kuwa alianza Kuonekana tokea mwaka juzi akiwa bado Mdogo baada ya Kutupwa huko Porini ( Msituni ) Lugalo na Wasukuma waliokuwa wakiwafuga wengine na kuwatumia katika Ngoma zao za Kitamaduni.

Watu wengine wanasema kuwa kuna uwezekano Chatu huyo akawa ameletwa na Maji ya Mto Mlalakuwa yanayopita hadi jirani na Kambi ya Lugalo, kule Golf Club mpaka JKT Mlalakuwa hivyo akanasa na kuamua kuanza Maisha yake eneo hilo.

Katika hali isiyokuwa ya Kawaida baada ya Watendaji wa Serikali ya Mtaa Kawe ( yenye Ofisi zake jirani na Soko jipya la Kawe ) walipotaarifiwa 'walijitutumua' kutaka kuonyesha 'Ushujaa' ambao hawana kwa kuamua kwenda 'Kavu Kavu' huko Msituni ( Porini ) Lugalo ( zamani Hostel ) ili Kumdhibiti.

Ila walipofika huko na Kumuona ndani ya dakika Moja mpaka Mbili hakuna aliyebakia hapo ambapo wote 'walitimka mbio' kwa kila Mtu kupita njia anayoijua ila Wote wakaja kukutania Ofisini huku wote wakiwa wameshika Viatu vyao Mikononi na wengine wakiomba Funguo za kwenda Msalani ( Chooni ) kujikagua kama wakati wakikimbia vile kwa Uwoga wa Kumuona Chatu labda kwa kutokujua ( Kihoro ) walijisaidia 'Kibaiolojia' vile walivyovihifadhi katika 'Vitambi' vyao.

Tafadhali naziomba Mamlaka husika hasa ya Jeshi ( JWTZ ) na Serikali ( kupitia Maliasili ) kulifuatilia hili upesi na Kumtoa upesi huyo Chatu hapo Porini ( Msituni ) kwani wengine ( GENTAMYCINE ) katika hayo Makaburi ( ya zamani Hostel ) nimemzika Mama yangu Mdogo na nilikuwa napanga kwenda 'Kumfagilia' na Kumsalimia 'Kimaombi' Siku za Usoni.

Lakini Taarifa hii imenishtua na Kuniogopesha kwenda huko ili Chatu asije 'Kuupiga Mwingi Kwangu' na nikawa Historia hapa JamiiForums na hata nikaikosa 'Derby' ya Jumapili ijayo huko Mkoani Kigoma ambapo najua Mugalu, Boko, Chama, Kagere na Miquissone wanaenda 'Kuninyooshea' na Kunifundishia Watu Adabu kwa Kipigo cha Mwana Ukome.

Kwa wale wenye Blogs zenu na Media zingine mbalimbali tafadhali siwazuii Kuichukua hii Taarifa yangu na Kuitumia ila nawaomba tu mkiitumia toeni 'Credit' kwa Mtandao huu wa JamiiForums na Mimi GENTAMYCINE niliyeileta ( iweka wazi ) na acheni Kudanganya kuwa mmeitafuta nyie kwani mnakuwa hamtendi Haki na Kutuvunja Moyo Watu tunaopenda Kutafuta Taarifa na Kuzianzishia hapa JamiiForums mzijue hata kama hakuna tunacholipwa ila tunajua tutalipwa vikubwa ( zaidi ) na Mwenyezi Mungu Siku moja atakayoipenda na kuichagua Yeye.
Umefanya vizuri kutoweka picha hapa,

Kuna member mmoja humu huwa anawatetea sana hao wadudu, apatapo ujumbe huu akamchukue
 
Inasikitisha sana!! Wasimuue wamkamate na kumpeleka zoo ,yule mwanajeshi aliyemuua chatu inatakiwa akamatwe! Lugalo nimekaa ila Hostel sisijui zipo wapi.
Mkuu unaniangusha bhana yaani unasema umekaa Lugalo halafu Hostel hupajui?

Hostel ni kule ambako zamani walikuwa wakiishi sana wale Askari Wahanga wa Vita ya Amini wa Uganda ( wengi wao wakiwa ni Vilema ) nyuma yake kuna Makaburi ila kwa sasa ndipo Kumejengwa Chuo Kikubwa cha Tiba cha MCMS kwa Ushirikiano na nchi ya Ujerumani ambapo kuna VIP Mortuary ambayo Hayati wa tarehe 17 Machi, 2021 alikuwa akilala na akiogeshewa hapo kabla ya kupelekwa Temeke Main Stadium Watu Kumuaga.
 
Mungu ameagiza tumuue nyoka, kosa kumuua nyoka mbugani ila hapo alipo anatishia uhai wa maisha ya watu
Mungu Kwake Mbinguni na Serikali nayo Kwake ni hapa duniani. Huyu Chatu wajitahidi tu wamtoe tena kwa Kumdekeza na Kumbembeleza kisha wakamuweke huko Mbugani ila siyo kwa Kumuua kwani nasikia Kisheria hata akiwa wapi au akija Kukutembelea Kwako ukimuua tu tayari una Kesi na Jamhuri kwa kuharibu Nyara yake.
 
Mkuu unaniangusha bhana yaani unasema umekaa Lugalo halafu Hostel hupajui?

Hostel ni kule ambako zamani walikuwa wakiishi sana wale Askari Wahanga wa Vita ya Amini wa Uganda ( wengi wao wakiwa ni Vilema ) nyuma yake kuna Makaburi ila kwa sasa ndipo Kumejengwa Chuo Kikubwa cha Tiba cha MCMS kwa Ushirikiano na nchi ya Ujerumani ambapo kuna VIP Mortuary ambayo Hayati wa tarehe 17 Machi, 2021 alikuwa akilala na akiogeshewa hapo kabla ya kupelekwa Temeke Main Stadium Watu Kumuaga.

Okay nimekaa ukwamani na Lugalo kwa juu kule kwenye ukumbi wa sherehe ,huwa napita njia ya posta lugalo kushuka chini darajani kufanya matizi.
 
Huu uandishi watu wengi kuuelewa watapuyanga hatari, sijui tuwafumbue macho waelewe maada au tukaushe wapate picha ya chatu vichwani mwao?
 
Chatu kupambana nae inahitaji watu majasiri sana
Na 99% ya Watendaji wa Serikali za Mitaa wa hapo Kawe Mzimuni hadi Walinzi Shurikishi achilia mbali Polisi wa Kawe Kituoni hakuna ninayemuona ni Jasiri wa Kupambana na huyo Chatu Mkuu ukizingatia Watu wote hawa nawajua tena ni Waoga hata mara mbili yangu.

Kuna Mmoja wao ni Mnene sana nasikia nae juzi katika hiyo Ziara ya Msako wa huyo Chatu nae 'alijitutumua' kwenda tena akiongoza Msafara ila kwa jinsi alivyopotea ghafla kwa Kutimka mbio kule Porini Lugalo Chuo cha Udaktari ( MCMS ) amethibitisha kuwa Watu Wanene ( Vibonge ) kwenye Shida huwa wanakimbia hata Usain Bolt anasubiri.
 
Mungu Kwake Mbinguni na Serikali nayo Kwake ni hapa duniani. Huyu Chatu wajitahidi tu wamtoe tena kwa Kumdekeza na Kumbembeleza kisha wakamuweke huko Mbugani ila siyo kwa Kumuua kwani nasikia Kisheria hata akiwa wapi au akija Kukutembelea Kwako ukimuua tu tayari una Kesi na Jamhuri kwa kuharibu Nyara yake.
Mkuu unatumia tafsida nini? Ukute unazungumzia kitu kingine mimi nahisi chatu mnyama, kama ni chatu hakuna kosa kumuua, juzi tu kuna mjeda kaua chatu pekeyake na habari ipo youtube na kwa milad ayo
 
Okay nimekaa ukwamani na Lugalo kwa juu kule kwenye ukumbi wa sherehe ,huwa napita njia ya posta lugalo kushuka chini darajani kufanya matizi.
Kama umekaa Kawe Ukwamani basi ni lazima tu utakuwa ni Mchawi sana au tayari una Vimelea vyote 'tukuka' vya Uchawi ( Ndumbaism ) kwani kwa Dar es Salaam nzima Makao Makuu ya Uchawi ni hapo Kawe Ukwamani kisha wakifuatiwa kwa ukaribu sana na Mbagala, Tandale, Vingunguti, Tandika na Kunduchi Mtongani.
 
Maeneo ya jeshi pale Kawe ni makubwa sana!! waanzishe zoo!! hapo hapo!! hkn shida watu tule viingilio!! tutaishije sasa!! jeshini siyo wabunifu!!
mleta mada huyu mkurya huyu? siyo alizikaje mama ake pale kwa wajeda??? mitoto ya kapiteni wewe kwani??
 
Mimi ni mkazi wa kawe hapa Joseph, hizo story za chatu nimemekua nikizisikia tuu kama hekaya hivii.

Maana wengi wanao mzungumzia huyo chatu ni wamesikia tuuu, hakuna alie muonaa.

Maana wazee wetu wa kawe nao hawana jambo dogoo, usikute wana yakoo
 
Back
Top Bottom