Baada wa Watendaji wa Serikali za Mitaa Kawe 'Kutimka Mbio' Kuogopa 'Chatu' aliyeko katika pori la Chuo cha Tiba Lugalo msaada unahitajika

Unapokuwa mgeni nchi za watu jitahidi kuwaheshimu wenyeji POPOMA wewe, mbona watz wakifika kigali na bujumbura wanakuwa na heshima?
 
Umefanya vizuri kutoweka picha hapa,

Kuna member mmoja humu huwa anawatetea sana hao wadudu, apatapo ujumbe huu akamchukue
 
Inasikitisha sana!! Wasimuue wamkamate na kumpeleka zoo ,yule mwanajeshi aliyemuua chatu inatakiwa akamatwe! Lugalo nimekaa ila Hostel sisijui zipo wapi.
Mkuu unaniangusha bhana yaani unasema umekaa Lugalo halafu Hostel hupajui?

Hostel ni kule ambako zamani walikuwa wakiishi sana wale Askari Wahanga wa Vita ya Amini wa Uganda ( wengi wao wakiwa ni Vilema ) nyuma yake kuna Makaburi ila kwa sasa ndipo Kumejengwa Chuo Kikubwa cha Tiba cha MCMS kwa Ushirikiano na nchi ya Ujerumani ambapo kuna VIP Mortuary ambayo Hayati wa tarehe 17 Machi, 2021 alikuwa akilala na akiogeshewa hapo kabla ya kupelekwa Temeke Main Stadium Watu Kumuaga.
 
Mungu ameagiza tumuue nyoka, kosa kumuua nyoka mbugani ila hapo alipo anatishia uhai wa maisha ya watu
Mungu Kwake Mbinguni na Serikali nayo Kwake ni hapa duniani. Huyu Chatu wajitahidi tu wamtoe tena kwa Kumdekeza na Kumbembeleza kisha wakamuweke huko Mbugani ila siyo kwa Kumuua kwani nasikia Kisheria hata akiwa wapi au akija Kukutembelea Kwako ukimuua tu tayari una Kesi na Jamhuri kwa kuharibu Nyara yake.
 

Okay nimekaa ukwamani na Lugalo kwa juu kule kwenye ukumbi wa sherehe ,huwa napita njia ya posta lugalo kushuka chini darajani kufanya matizi.
 
Huu uandishi watu wengi kuuelewa watapuyanga hatari, sijui tuwafumbue macho waelewe maada au tukaushe wapate picha ya chatu vichwani mwao?
 
Chatu kupambana nae inahitaji watu majasiri sana
Na 99% ya Watendaji wa Serikali za Mitaa wa hapo Kawe Mzimuni hadi Walinzi Shurikishi achilia mbali Polisi wa Kawe Kituoni hakuna ninayemuona ni Jasiri wa Kupambana na huyo Chatu Mkuu ukizingatia Watu wote hawa nawajua tena ni Waoga hata mara mbili yangu.

Kuna Mmoja wao ni Mnene sana nasikia nae juzi katika hiyo Ziara ya Msako wa huyo Chatu nae 'alijitutumua' kwenda tena akiongoza Msafara ila kwa jinsi alivyopotea ghafla kwa Kutimka mbio kule Porini Lugalo Chuo cha Udaktari ( MCMS ) amethibitisha kuwa Watu Wanene ( Vibonge ) kwenye Shida huwa wanakimbia hata Usain Bolt anasubiri.
 
Mkuu unatumia tafsida nini? Ukute unazungumzia kitu kingine mimi nahisi chatu mnyama, kama ni chatu hakuna kosa kumuua, juzi tu kuna mjeda kaua chatu pekeyake na habari ipo youtube na kwa milad ayo
 
Okay nimekaa ukwamani na Lugalo kwa juu kule kwenye ukumbi wa sherehe ,huwa napita njia ya posta lugalo kushuka chini darajani kufanya matizi.
Kama umekaa Kawe Ukwamani basi ni lazima tu utakuwa ni Mchawi sana au tayari una Vimelea vyote 'tukuka' vya Uchawi ( Ndumbaism ) kwani kwa Dar es Salaam nzima Makao Makuu ya Uchawi ni hapo Kawe Ukwamani kisha wakifuatiwa kwa ukaribu sana na Mbagala, Tandale, Vingunguti, Tandika na Kunduchi Mtongani.
 
Maeneo ya jeshi pale Kawe ni makubwa sana!! waanzishe zoo!! hapo hapo!! hkn shida watu tule viingilio!! tutaishije sasa!! jeshini siyo wabunifu!!
mleta mada huyu mkurya huyu? siyo alizikaje mama ake pale kwa wajeda??? mitoto ya kapiteni wewe kwani??
 
Mimi ni mkazi wa kawe hapa Joseph, hizo story za chatu nimemekua nikizisikia tuu kama hekaya hivii.

Maana wengi wanao mzungumzia huyo chatu ni wamesikia tuuu, hakuna alie muonaa.

Maana wazee wetu wa kawe nao hawana jambo dogoo, usikute wana yakoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…