Baada ya Airtel kuthibitika kutumika kisiasa, wateja tusitumie Airtel Money, ukiweza itupe line au uipumzishe

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Imeelezwa kuwa CHADEMA ilikuwa ikikusanya michango ya wanachama kwaajili ya maadhimisho ya 33 tangu kuanzishwa kwake, kwa kutumia huduma ya Airtel Money. Huku michango ikiwa inaendelea, Airtel baada ya kupokea maelekezo kutoka chama kile cha mauaji na serikali yake, wameamua kuifungia hiyo line iliyokuwa ikitumika kukusanya michango.

Hii inatupatia ujumbe muhimu kuwa hata taasisi za huduma nchini mwetu zimeharibiwa, na sasa zinatumika kama jumuiya za chama, sawa ilivyo UVCCM au UWT.

Kwa kuwa Airtel wamejidhihirisha wazi pasipo shaka kuwa wao siyo taasisi ya kibiashara bali ni genge la wahuni wa kile chama kilichoendesha mauaji ya zaidi ya wananchi 10,000; tusiounga mkono uharamia ule, tusitumie huduma za Airtel, kwani hawa wamethibitisha kuwa siyo kampuni ya mawasiliano bali ni wahuni wa kisiasa wanaoendesha uhuni wao kupitoa huduma ya mawasiliano. Hii pia inatuletea ujumbe kuwa kama wewe ni mtumiaji wa Airtel, ikitokea wale wauaji wakawa wanakutafuta, hawa Airtel wanaweza kutumika katika kufuatilia uko wapi.

Wito
Kwa usalama wako, usitumie mtamdao wa Airtel. Tuwasusie, japo kwa miezi hata 6, tuone kama watajirekebisha. Usikubali kumtumia mtu hela anayekupa line ya Airtel, mwombe akupatie namba ya mtandao tofauti. Na wewe mwenyewe, kama una line nyingine, Airtel iache ipumzike, isije ikakuangamiza.
 
Hizi ndo akili za CHADEMA
 
Kama huwezi kutumia Airtel kwa sababu ya udukuzi wa Serikali, basi usimiliki laini ya simu yeyote. Ishi kama walivyoishi mababu zetu.

Hakuna kampuni ya simu yeyote inayoweza kukataa kutoa maelezo kwa Serikali pale ambapo Serikali inataka.

Hata wenye makampuni wanajuwa kabisa kuwa kufanya biashara Tanzania ni privilege na siyo haki.
 
Hizo campaign zenu za kipuuzi hamjaanza leo na hamtafanikiwa.
Mnasahau mapema sana wazee wa kudandia kila jambo.
Umeisahai ile kampeni yenu dhidi ya Vodacom!
 
Kutoa ushirikiano kwa serekali kuhusu uhalifu hiyo ni sahihi, je hiyo namba imefanya uhalifu gani hadi serekali iwaagize Airtel waifungie?

Hakuna kitu kigumu kama kulazimisha kuongoza watu waliokuchoka. Ni sawa na mwanamke aliyezeeka lakini anajipodoa na kuvaa nguo fupi ili aendelee kupendwa na wanaume. Matokeo yake akikataliwa anaanza kuwafanyia figisu wasichana wadogo wanaokubalika. Ccm wakubali tu hiki si kizazi chao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…