The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Dkt.Juma Homera ametembelea na kukagua barabara ya Mlima iwambi na barabara ya mchepuo ya muda kwaajili ya kupita Magari kupishana na Malori.
Dkt.Homera amesema hapo awali walitoa agizo la magari makubwa yapite njia ya mchepuo lakini baada ushauri wa wadau mbalimbali wamepokea mapendekezo yao na kuagiza Malori yapite barabara kuu na magari madogo yapite barabara ya mchepuo ili kutoleta madhara ya mara kwa mara ya ajali.
Dkt.Homera amesema tayari bilioni tatu zimekwishalipwa kwa wananchi kama fidia ili wapishe ujenzi wa njia nne uanze mara moja eneo la mlima iwambi.