Nadhani kwa Tanzania tatizo ni ccm
CCM ni tatizo kubwa lakini cha ajabu tuna wapinzani wenye wivu na uhasama mkubwa kwao wenyewe kuliko walio nao kwa CCM .
Mfano tu ni hulka ya kike na utoto aliouonyesha Mbowe .Mtu tuliyekua tunajua kuwa anaichukia CCM kuliko hata anavyomchukia Shetani asiyejulikana kwenye mambo ya siasa na tawala zinye katiba zisizo za kidini kama Tanzania ,baada ya kuchukua fomu kwa hasira eti Lisu amesema amekosoa baadhi ya mifumo kwenye katiba ya chadema na pia kusema kuwa atahakikisha mfumo wa upatikanaji wa fedha na matumizi yake unakua wa kitaasisi na sio mtu binafsi.
Yaani hayo tu akafura kwa hasira na kuchukua fomu ili atumie mwanya huo kujibu mapigo na kusema kuwa amapambaniq sana chama kwa mali zake ,anajitolea kwa mali zake,uongozi wa kisiasa ni mzigo mzito 😂😂😂😂. Sasa mzigo mzito unaungangania wa nini wakati umepata mtu wa kukusaidia 😂😆😆.
Tunamuona kwa dhahiri na genge lake kuwa hawana nia ya kuitoa CCM madarakani mana Madai ya Lisu ndiyo yaliyokuwa yanatumiwa na CCM kwenye kampeni zao kuwaonyesha wananchi kuwa Chadema ni mali ya Mbowe na Sacoss yake ya kujipatia pesa ,lakini pia Suala la Uenyekiti wa chama ni suala la milele kwa Mbowe na mtu yeyote anayejitokeza kugombea anakua ni adui na anaweza hata kupoteza maisha yake . Na pia suala la ukabila lilikua minatajwa sana na CCM na kufanikiwa kuifanya Chadema idumae na kukosa wanachama wapya wasio na vyama .
Tumitegemea Mbowe awe mkomavu wa kisasa na kumuunga mkono Lisu ili wapangue hoja za CCM na kuwaonyesha kwa vitendo kuwa madai yao sio ya kweli . Kwa sababu mtu yeyote anayegombea nafasi ni lazima ajibu maswali ya kwa nini anataka nafasi hiyo na wapi kuna mapungufu ili kuonyesha kuwa hagombei kwa uroho wa madaraka tu au eti kumrithi kiongozi aliyepo .Huu sio utawala wa kifamilia au kifalme wa kurithi tu kama mali ya mtu.
Kikwete angekua na hasira za Mkisi kama Mbowe angeweza kufuta uchaguzi na kuongeza muda wa kukaa madarakani alipoona Lowasa amehama chama ,lakini pia aliposikia Magufuli anasema atawashughulikia mafisadi na majibu yaliyopo CCM . Na paka kusema kuwa serikali iatkayo kuja ni serikali ya Magufuli badala ya kusema ni serikali ya CCM . JK kwa
ukomavu na uelewa wa siasa za kidemokrasia aliangalia taifa ,chama na akaendelea na kumpigia kampeni JPM na kusema kuwa anatema Cheche .
Mbowe angeonyesha ukomavu na busara kwa ajili ya kukilinda chama na kurejesha imani kwa watanzania kuwa wamepata mtu wa kukihuisha chama .
Badala yake anasifia 4R ya kihuni . Mtu anakuruhusu fanya mikutano halafu unatumia gharama kubwa kufanya mikutano kisha uchaguzi ukifika anavuruga uchaguzi na mkilalamika mtu yule yule anatuma majeshi na watu katili wanakuja kuua WATU wako na kukamata wagombea na kupigwa na kuumizwa .Sasa Lisu alikosoa hiyo 4R anakua ni adui kuliko CCM na usanii wao wa 4R ya kuwahadaa wananchi .
Mbowe anajazwa sifa za kijinga kuba ana busara na lisu hana Busara . Hivi busara inatakiwa ifanywe na wapinzani tu na sio CCM ? Kwa nini Mbowe haoni uchafuzi na uhuni wa CCM kwenye uchaguzi kuwa huko ndiko kukosekana kwa Busara na sio lisu anayepinga uonevu.
Mara nyingi Lidu amehudhuria kwenye Misiba ya watu waliouawa kule Singida mpaka wakiwepo wakuu wa wilaya lakini hajawahi kutoa hotuba zenye kujenga hasira na chuki kama ile hatuna ya Mbowe kule Tanga iliyosababisha watu kutaka kumpiga Waziri Madini ! Wapumbavu hawakuona kuwa aliyechochea vurugu alikua ni Mbowe na akajifanya kutuliza vurugu aliyoianzisha yeye. Sasa ile ni busara au usanii ?
Lakini pia aliyeua 4R sio Lisu ni Mbowe mwenyewe siku alipokosa Busara kwenye msiba wa Ally Kibao na kuitisha maandamano ya kumfukuza Rais Dr.Samia Madarakani. Hapa ndipo alipoondoa 4R yeye mwenyewe na sio Lisu. Hapo busara bandia ya Mbowe ililingana na busara ya Dr.Samia 😂😂😂😂😂😂😂Moto ukawaka na mapembe yakakatwa . Sasa hapo nani mkurupukaji kama sio Mbowe . Lisu alihusika vipi kuvunja 4R
Kwa nini tunakubali kudanganywa na CCM ili kumrudisha Mbowe kwenye kiti wapate uchochoro kwenye uchaguzi ujao ?