Baada ya Angalizo UN, Katiba Mpya - Mapambano yanaendelea

Baada ya Angalizo UN, Katiba Mpya - Mapambano yanaendelea

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hii ni habari njema kutokea UN. Uthibitisho zaidi kuwa ni nini iliyo kiu ya watu kote duniani.

Tusidanganyane tunataka kupumua kwa uhuru, haki na usawa kisiasa na kijamii.

Kiongozi dikteta si wa zama hizi.

Hautakuwa peke yako baba askofu.

Zambia wametambuliwa kwa jitihada zao za kujenga demokrasia. Tuko katika njia salama. Kasema rais wa dunia wako tayari kujadiliana na kuwaunga mkono wapigania demokrasia kote duniani.

Pamoja na yote hatuko peke yetu na SSH ameambiwa hivyo kama mjumbe rasmi mkutanoni.

Aluta Continua!
 
Si mlitoka wenyewe kwenye bunge la katiba, kwani mlilazimishwa kutoka?

Umemsikia rais wa dunia?

“The future belongs to those who give their people the ability to breathe free, not those who seek to suffocate their people with an iron hand authoritarianism."

Chief Hangaya kesha kupa mrejesho?
 
Ni mamemo ya matumaini makubwa mno kutoka kwa Rais Biden, ni muda sasa wa marais wa kiafrica kukaa chini na kutafakari...kuachana na kutamka maneno matamu yenye matumaini ya kukuza demokrasia na utawala bora huku matendo yao yakiwa ni kinyume kabisa.

"The future belongs to those who make their people to breathe free and not whose who seek to suffocate their people on their own hands. " Thank you Mr. Biden.
 
Umemsikia rais wa dunia?

"The future belongs to those who leave their people to breathe freely. Not those who suffocate them with an iron hand."

Chief Hangaya kesha kupa mrejesho?
Uliisha ambiwa sio coca cola

Mnajifanya machizi tu hamsikii, eti rais wa dunia!!!!
 
Fanya Fujo Uone (FFU)
FFU, moja ya marungu ya dola ambayo ccm iliyofilisika inayatumia kubaki madarakani. Ilishapoteza uhalali wa kisiasa. Siku zote ndio jibu la ccm kwa harakati za vyama vya siasa, ambavyo hutumia njia halali za ushawishi kwa jamii. Na pia ni kwa mujibu wa Katiba na sheria ya vyama vya siasa. CCM inajua fika kwamba kama itaingia uwanja wa siasa kupambana kisiasa, haifui dafu siyo tu kwa vigogo wa siasa za Tanzania , CHADEMA , bali hata kwa vyama njaa kama "Demokrasia Makini".
 
Ukiangalia hako kakofia ka askofu wenu utajua mmeisha pigwa hapo hamna kitu.
Huyo ni kiongozi wa kiroho mkuu. Kama huelewi maana hasa ya hiyo kofia, bora unyamaze. Ila Tanzania tuna kasumba. Shehe, Askofu, Kardinali, au mchungaji yeyote akijiingiza katika siasa upande wa CCM, anaonekana ana busara. Ila akiingia upande wa upinzani, anaonekana ana mushkeli.
Upande wa upinzani kuna mateso ya kila aina. Kunyanyaswa, kashfa, kukamatwa, kuwekwa magerezani, hata kuuwawa. La kutia matumaini ni kwamba hayo yote yalimkuta pia Bwana Yesu. Na jinsi vile Bwana Yesu alitukuzwa baada utimilifu wa mateso, hawa nao watainuliwa juu,
 
Usimfananishe Yesu na mambo ya kipumbavu. Kwanza Yesu hakujihusisha na siasa alisema wazi utawala wake si wa dunia hii bali wabinguni.
 
Usimfananishe Yesu na mambo ya kipumbavu. Kwanza Yesu hakujihusisha na siasa alisema wazi utawala wake si wa dunia hii bali wabinguni.

Mambo ya kipumbavu ni utawala wa dunia hii?

Kwa hakika ya akina Kingai na wote wenye kushadadia kunyimana kupumua kana kwamba wao ni wakazi wa kudumu wa dunia hii ni ya kipumbavu sana.

Mambo ya kipumbavu hivi ni wajibu wetu na wapenda haki wote kuyapiga vita kwa nguvu zetu zote.

Cc: jiwe, Hangaya
 
Back
Top Bottom