BAADA ya msanii wa filamu Salma Jabu Nisha, kulitaka Baraza la Sanaa la Taifa BASATA, kumchukulia hatua kali msanii Aunty Ezekiel kwa madai picha zake za nusu utupu zinachafua maadili na kuwafanya wasanii wote waonekane wahuni,
naye amekuja juu na kumtaka Nisha afanye mambo yake na aache tabia ya kumfuatilia...
Ezekiel alidai kuwa haoni sababu ya Nisha, kumtolea maneno hayo kwani hata yeye ana matatizo yake hivyo anatakiwa kujichunguza yeye ndipo aende kwa mtu mwingine.
Alidai kwa sasa anatumia lugha ya kistaarabu zaidi yani haitaji bifu lakini akizidi kumfuatilia atachanua makucha, ingawa hana tabia ya kuchukuiana na mtu ila kwa hili hajakubaliana nalo kwani wapo wasanii wagapi wanakosea na hajawahi kutoa kauli kama hiyo.
Hata hivyo aliongeza kuwa asitake kutumia kauli za mpenzi wake Ney, kuwa makahaba wako bongo movie kwani hata mwenyewe ni mmoja wa wasanii wa tasnia hiyo.