Kwanza poleni na msiba
Twende kwenye mada, nitakupa ushauri/mwanga wa juu kuhusu wa sheria za mirathi japo hujasema nyie ni dini gani ila ipo hivi;
1. Kanuni ya kwanza kuifahamu ni kuwa, hauwezi kudai mirathi ambayo angerithi marehemu. Ufafanuzi ni kuwa mtu hawezi akadai apatiwe mali ambayo ingerithiwa na mtu mwingine kama uyo mtu angekywa hai.
Mfano, mtoto hawezi kudai urithi wa mzazi wake ambaye ni marehemu. Kama nimekuelewa vizuri hawa ndugu zenu wanadai malu ambayo kama mama yao angekuwa hai basi angerithi kutoka kwa baba yenu mara baada ya baba yenu kufariki.
Kama ni hivyo, basi hilo haliwezekani kisheria. Marehemu anakufa na haki/urithi wake.
2. Kanuni ya pili ni kila mtoto ana haki ya kurithi kutoka kwa baba yake. Sheria ya mirathi kwa sasa haibagui mtoto yeyote wa marehemu. Awe kazaliwa ndani ya ndoa au alizaluwa kutokana na baba yake kuchepuka.
Kisheria hakuna mtoto haramu, wote ni watoto wenye haki sawa.
Sasa hawa ndugu zenu wanaweza kutumia msimamo huu wa kisheria kudai urithi wao kutoka kwa baba yao ambaye ni baba yenu pia. Hii haihitaji ushauri zaidi ya kukwambia kuwa ni haki yao kisheria na wanaweza kuitekeleza.
Hapa kuna jambo muhimu sana la kufanya ilimali za marehemu zisipotee holela.
Ili kuepusha migogoro hapo baadae nawashauri mfungue mirathi katika mahakama ya mwanzo iliyopo eneo lenu. Ni rahisi sana na gharama nafuu, mtatakiwa mfanye yafuatayo kabla hamjaenda mahakamani kufungua mirathi
1. Mnatakiwa mtafute wosia aluoacha marehemu baba yenu. Kama hajaacha wosiana kabisa fuateni hatua ya pilihapo chini
2. Mnatakiwa kufanya kikao cha familia kumchagua msimamizi wa mirathi, huyu ndio atagawa mali za marehemu kama ataidhinishwa na mahakama
3. Baada ya kufanya kikao cha kumteua msimamizi wa mirathi, andaeni muhktasari muupeleke mahakama ya mwanzo ambapo mtafungua shauri la mirathi (huu sio ugomvi, ni taratibu tu).
4. Baada ya kufungua mirathi litatoka tangazo la kuomba kuwa msimamizi wa mirathi na kama hakutakuwa na pingamuzi lolote basi mahakama itamuidhinisha huyo mliyemchagua kuwa msimamizi wa mirathi, na atatakiwa kujaza fomu ya wadhamini mahakamani.
Baada ya hapo ataanza kazi ya kukusanya na kugawa mali za marehemu kwa warithi wote, hapa ni muhimu mtambue kuwa kwa sasa warithi wanaoonekana wazi ni watoto na mke aliye hai (kama ana cheti cha ndoa) yule mke aliyekwisha fariki sio mrithi.
Baada ya kukamilisha kugawa mali kwa warithi, msimamizi wa mirathi atapeleka hesabu mahakamani kwa ajili ya kufunga mirathi. Na mahakama itafanta hivyo.
NB: Kama hakuna migogoro ni zoezi la muda mfupi sana miezi mi 3, ila kama kuna migogoro linaweza likawa zoezi la hadi miaka 20, ni nyie tu mchague liwe zoezi fupi au refu
Kila la kheri, natumaini umepata mwanga. Ukiwa na swali uliza Mkuu.