crankshaft
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,427
- 3,438
Wanaweza kurithi urithi wao hata kama mama yao yupo hai kwani na yeye (mama yao) atapewa urithi wake kama wakifungua mirathi mahakamani.Mkuu wala sio lazima digrii ya sheria hapo. Hao watoto wanayo haki yao hapo.
Kuwa hai kwa mama yenu ni jambo jema ila wao uhusiano wao ni baba sio mama yenu. Nyinyi ndo hamuwezi uliza urithi sababu mama yenu bado yupo.
Kama nimemuelewa tofauti?? Kwamba hao watoto ni baba mwingine si baba mmoja na wao.Baba yenu mmoja halafu mnataka kujifanya nyie ndio mna haki juu ya wenzenu, sio uungwana huo.
Hawawezi kutoa mali yoyote sababu wao sio mahakama, mirathi inasimamuwa na mahakama tu, nje ya hapo ni batili na inaweza kusababisha migogoro isiyoisha. Na hapa ndipo watu wengi wanashindwa kujua na kutumbukia mtegoniToeni mali ya mama yenu aliyochuma na mume. 50% ya mama yenu ikitoka hizo zingine gawaneni.
Kugawana ni desturi ya mitoto mipumbavu inayopatikana kusini mwa jangwa la Sahara.
Subhanallah! Wewe ndio umenifanya nikamsome tena,Kama nimemuelewa tofauti?? Kwamba hao watoto ni baba mwingine si baba mmoja na wao.
Umefafanua vema lakini kumbe hatukumuelewa Mtoa Mada, yeye alimaanisha hao Watoto wana Baba yao kwa maana Mama yao aliolewa na Baba yao akiwa tayari amezaa kwengine,Kwanza poleni na msiba
Twende kwenye mada, nitakupa ushauri/mwanga wa juu kuhusu wa sheria za mirathi japo hujasema nyie ni dini gani ila ipo hivi;
1. Kanuni ya kwanza kuifahamu ni kuwa, hauwezi kudai mirathi ambayo angerithi marehemu. Ufafanuzi ni kuwa mtu hawezi akadai apatiwe mali ambayo ingerithiwa na mtu mwingine kama uyo mtu angekywa hai.
Mfano, mtoto hawezi kudai urithi wa mzazi wake ambaye ni marehemu. Kama nimekuelewa vizuri hawa ndugu zenu wanadai malu ambayo kama mama yao angekuwa hai basi angerithi kutoka kwa baba yenu mara baada ya baba yenu kufariki.
Kama ni hivyo, basi hilo haliwezekani kisheria. Marehemu anakufa na haki/urithi wake.
2. Kanuni ya pili ni kila mtoto ana haki ya kurithi kutoka kwa baba yake. Sheria ya mirathi kwa sasa haibagui mtoto yeyote wa marehemu. Awe kazaliwa ndani ya ndoa au alizaluwa kutokana na baba yake kuchepuka.
Kisheria hakuna mtoto haramu, wote ni watoto wenye haki sawa.
Sasa hawa ndugu zenu wanaweza kutumia msimamo huu wa kisheria kudai urithi wao kutoka kwa baba yao ambaye ni baba yenu pia. Hii haihitaji ushauri zaidi ya kukwambia kuwa ni haki yao kisheria na wanaweza kuitekeleza.
Hapa kuna jambo muhimu sana la kufanya ilimali za marehemu zisipotee holela.
Ili kuepusha migogoro hapo baadae nawashauri mfungue mirathi katika mahakama ya mwanzo iliyopo eneo lenu. Ni rahisi sana na gharama nafuu, mtatakiwa mfanye yafuatayo kabla hamjaenda mahakamani kufungua mirathi
1. Mnatakiwa mtafute wosia aluoacha marehemu baba yenu. Kama hajaacha wosiana kabisa fuateni hatua ya pilihapo chini
2. Mnatakiwa kufanya kikao cha familia kumchagua msimamizi wa mirathi, huyu ndio atagawa mali za marehemu kama ataidhinishwa na mahakama
3. Baada ya kufanya kikao cha kumteua msimamizi wa mirathi, andaeni muhktasari muupeleke mahakama ya mwanzo ambapo mtafungua shauri la mirathi (huu sio ugomvi, ni taratibu tu).
4. Baada ya kufungua mirathi litatoka tangazo la kuomba kuwa msimamizi wa mirathi na kama hakutakuwa na pingamuzi lolote basi mahakama itamuidhinisha huyo mliyemchagua kuwa msimamizi wa mirathi, na atatakiwa kujaza fomu ya wadhamini mahakamani.
Baada ya hapo ataanza kazi ya kukusanya na kugawa mali za marehemu kwa warithi wote, hapa ni muhimu mtambue kuwa kwa sasa warithi wanaoonekana wazi ni watoto na mke aliye hai (kama ana cheti cha ndoa) yule mke aliyekwisha fariki sio mrithi.
Baada ya kukamilisha kugawa mali kwa warithi, msimamizi wa mirathi atapeleka hesabu mahakamani kwa ajili ya kufunga mirathi. Na mahakama itafanta hivyo.
NB: Kama hakuna migogoro ni zoezi la muda mfupi sana miezi mi 3, ila kama kuna migogoro linaweza likawa zoezi la hadi miaka 20, ni nyie tu mchague liwe zoezi fupi au refu
Kila la kheri, natumaini umepata mwanga. Ukiwa na swali uliza Mkuu.
Hapana Mkuu labda ni nukuu maelezo yake kasema hivi; ''Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu na mdogo alikuwa ana watoto wake'' hiyo kauli alikuwa na watoto wake ameitumia sababu mbele amekuja kusema kuwa huyo mke mdogo amekwisha fariki.Umefafanua vema lakini kumbe hatukumuelewa Mtoa Mada, yeye alimaanisha hao Watoto wana Baba yao kwa maana Mama yao aliolewa na Baba yao akiwa tayari amezaa kwengine,
Sasa hao Watoto wanataka urithi wa huyo Mzee kwa Mgongo wa Marehemu Mama yao sababu aliolewa (kama ilikua ndoa kweli) na huyo Mzee.
Kama ndoa ya kiislamu na mama ndio alianza kufa si amekimbia urithi hapo? Bila shaka hawana urithi ila kama baba ndiyo alianza kufa then wana haki ya alichostahili kupata mama yao. Full stop.Okay, kama ni Ndoa ya Kiislam na Bi Mdogo aliolewa kwa Ndoa hiyo basi hao Watoto waende Mahakamani watapewa muongozo
Ndio maana chini nikaweka angalizo,Kama ndoa ya kiislamu na mama ndio alianza kufa si amekimbia urithi hapo? Bila shaka hawana urithi ila kama baba ndiyo alianza kufa then wana haki ya alichostahili kupata mama yao. Full stop.
"Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu sisi na mdogo alikuwa ana watoto wake"Hapana Mkuu labda ni nukuu maelezo yake kasema hivi; ''Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu na mdogo alikuwa ana watoto wake'' hiyo kauli alikuwa na watoto wake ameitumia sababu mbele amekuja kusema kuwa huyo mke mdogo amekwisha fariki.
Hakuna sehemu kasema kuwa hao wadogo zao wana baba yao, labda kama ame edit uzi ila hadi sasa sijaiona Mkuu.
Kwa nilivyomuelewa mleta uzi ni kuwa baba yao ana wake wawili na wote wana watoto na baba yao. Sasa baba yao na mke mdogo tayari wamekwishafariki kabaki mke mkubwa ambaye pia ni mama wa mleta uzi.
Sasa kilichomfanya afungue uzi ni kuwa hawa watoto wa mke mdogo ambao ni wadogo zake wanataka mirathi ya marehemu mama yao kutoka kwa marehemu baba yao.
Mleta uzi inaonekana hana shida ma wadodo zake kudai mirathi yao ila shida ipo pale wanapodai mirathi ya mama yao kwa marehemu baba yao ili halu huyo mama yao naye ni marehemu. Sasa hapo ndipo alipohitaji kujua kisheria hiyo imekaaje?
Rudia taratibu kusoma uzi wake hasa ile aya ya kwanza kabisa Mkuu.
Anachoshangaa mleta uzi ni wao kudai mirathi ya mama yao ambaye ni marehemu. Yaani kwa maana nyingine ni kuwa wanadai haki ya marehemu mama yao kurithi mali kutoka kwa marehemu mume wake."Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu sisi na mdogo alikuwa ana watoto wake"
Labda ame edit lakini kusudio lake ndio hilo maana haiingii akilini kama watoto wazaliwe na baba mmoja halafu wawashangae wenzao kudai mirathi.
Nadhani mwenyewe angekuja aliweke hili jambo vizuri maana linachanganya,Anachoshangaa mleta uzi ni wao kudai mirathi ya mama yao ambaye ni marehemu. Yaani kwa maana nyingine ni kuwa wanadai haki ya marehemu mama yao kurithi mali kutoka kwa marehemu mume wake.
Ingekuwa wanadai mirathi yao wao kama watoto naamini mleta uzi asingeshangaa maana ni haki yao iyo hai.
Ishu hapo ni marehemu anadai vipi mirathi ya marehemu mwingine?, ambapo sheria ipo wazi kuwa marehemu hufa na urithi wakw kwenye mirathi yoyote aliyokuwa na haki nayo.
Mleta uzi ana swali zuri sana.