Baada ya Boniface Jacob kukamatwa na polisi bila kuzingatia sheria tujikumbushe sheria za ukamataji wa polisi (PGO)

Izia maji

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,997
Reaction score
5,385
ZIFAHAMU SHERIA ZA MSINGI UWAPO MIKONONI MWA POLISI

IMEANDALIWA NA MAWAKILI

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

SHARE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ILI WAZIFAHAMU HAKI ZAO
 
Hapo kwenye upekuzi
je? ni Askari wa cheo chochote anaruhusiwa kufanya upekuzi au nikuanzia cheo flan?
 
Si mlisema USA atazuia kuwakamata au?
 
Back
Top Bottom