Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 29,314
- 93,919
View: https://x.com/marxistJorge/status/1976999644975841453?s=19
"Watoto wetu wanahangaika sana , hayupo hapa Kuwaua wala kuwpaiga .Na sisi pia tunatipitia kile kile wanachopitia watoto wetu.Ni lazima tuwaunge Mkono " . TUSIKUBALI KUHADALIWA KWA PESA AU NAFASI ".
Haya ni Maneno ya Hasira na Uchungu kutoka Kwa Askari Wapiganaji wa Madagascar juu ya Gen Z.
Askari Hawa wamelitaka Jeshi la Polisi kuacha mara Moja kuwapiga Waandamanaji !!.
Gen Z kizazi ambacho kinaonekana kua na Akili na kugundua kua katika Nchi zao , Serikali zimewatupa
Ukosefu wa Ajira ,kukosekana Kwa Haki zao za msingi, Rasimali za Nchi zao zikitapanywa , Gen Z wakishuhudia Vijana wenzao ambao ni watoto wa Viongozi wakiyatanua Maisha Kwa Anasa , Ni wazi ilikua ni lazima Waanze kujitafuta!!.
Rais Rajoelina baada ya Maandamano ya wiki Kadhaa, anaamua kufuta Serikali yake , Lakini Gen Z hawapoi.
Anamteua Mkuu wa Majeshi kua Waziri Mkuu, hili linakua Kosa kubwa , hata Kwa mjinga ,anaona ni Rais Kaamua kumteua Mkuu wa Majeshi ili amsaidie Kuendelea kua MADARAKANI, Kwa kuamini AMRI na Maelekezo atakayotoa Kwa Viongozi wa Kijeshi wa Chini yake zitaliteka Jeshi na Kua Upande wake !!.
Sasa Jeshi ni la Askari wa Chini wasiokua na Vyeo, Jeshi sio la Askari wa Juu wachache ambao wanahongwa Kwa PESA NA NAFASI .
Wito : Wewe Mwanajeshi, Askari wa Chini, ambaye Pesa na NAFASI ulonayo vinaaksi Maisha ya kuhangaika anayopitia Mtanzania , Tarehe 29/10 na kuendelea ,Simama na Wananchi ,hili ni jambo la Wànanchi lenye Hatima ya Kulinda Rasimali za Nchi na Watu wake , hili ni Jambo la Wànanchi lenye lengo ya kurejesha Haki ,Ukweli na Uwajibikaji, Hili ni jambo la Wànanchi lenye lengo ya kurejesha Imani na Uhuru wa Kuabudu ,
Hili ni jambo la Wànanchi lenye lengo la kuhakikisha WAOVU WOTE Wanaotekwa watu, kuua, kufunga watu Kwa makesi ya Uongo wanafikishwa mbele ya sheria, Hili ni Jambo la Wànanchi lenye lengo la kuhakikisha Viongozi wote wanaotumia Nafasi zao vibaya, kufika Pesa ya Umma kujilimbikizia Utajiri na watoto wao , wakifikishwa katika Sheria, Hili ni jambo la Wànanchi ambalo lengo lake ni kuhakikisha Vijana wa Jeshini wanalipwa Mishahara mizuri zaidi kwakua Uwezo huo tunao na Rasimali zipo !!
Wanasiasa watakufa, ila Tanzania Itaishi !! Wanajeshi chondenchonde Tarehe 29/10 na kuendelea Msikubali Orders kutoka Kwa Seniors wenu zitakazowahitaji Kuwatis Ulemavu na Kuwaua kaka zenu, wadogo zenu ,mama zenu, dada zenu, wajomba, shangazi, rafiki na jamaa zenu, MSIKUBALI !!.
Utakapopewa ORDER hiyo ya kumvunja au Kumuua Mdogo wako alomazlia Chuo na Ajira hamna , kumbuka Familia ya Mafwele Iko South Afrika wanaponda Raha , kumbuka Watoto wa DGIS wanavyotaoanya Mabilioni ya Pesa za Kitanzania Kwa Anasa za Magari ya kifahari , Kumbuka Abdul anavyotapanya Pesa za WalipaKodi !!!.
Nchi hii, inaenda kua chini ya Vikwazo vya KIMATAIFA , Ulaya na Marekani vinaenda kusitisha Misaada na Mikopo, pale Hazina hamna Hela , IKIWA WANAJESHI mtakubali nanyinyi kuungana na Watesi kuwauliza Watanzania ,Kuanzia 2026 mtaishi Maisha magumu sana ,Kwa sababu kubwa Moja HAWATAKUA NA HELA YA KUENDESHA NCHI , WANATEGEMEA KUWAKAMUA WANANCHI KWELIKWELI !!.