nimekuwa nikishiriki jamiiforum km mgeni kwa muda mrefu sana. Kuna mengi mazuri km uhuru wa kuongea, kupashana habari, kujifunza na kuwafunza wengine, kuona misimamo na dhamira za watu mbalimbali, kuburudika na kufurahi.
Kuna mengine hayapendezi na yanachefua km lugha chafu, kughadhibika kwa baadhi na mawazo yakufuata mkumbo ya kiimani, kichama, na mengine km hayo huku ukweli na utashi ukisiginywa.
Pamoja na yote hayo hakukuwa na hakuna sehemu mtambuka km hii ambako watanganyika na wazanzibari wangeweza kukutanisha mawazo na fikra zao. Hivyo nimeona ni busara na hekima kuingia na kushiriki pamoja nanyi baada ya chabo za muda mrefu.
Nikaribisheni waungwana?