Baada ya Chama kugaragazwa Kura za Mchezaji Bora wa Wiki, ipi nafasi ya Simba Robo Fainali CAF?

Baada ya Chama kugaragazwa Kura za Mchezaji Bora wa Wiki, ipi nafasi ya Simba Robo Fainali CAF?

Simba akishinda haya mambo yanakua hayana maana .ila akishinda basi yanakua na maana
 
Mchezaji maachachari wa Al Ahly Mahmod Kahraba amemgaragaza Chama katika kuwania nafasi ya Uchezaji bora ya wiki. Ambapo Raia wa misri ambao wanashabikia timu hiyo walipiga kura na kumuwezesha kuibuka kinara.

Simba SC atamaliza nafasi ya pili kwenye kundi lake. Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni ni lazima apangiwe kucheza na washindi wa makundi mengine.

Washindi wa makundi mengine ambao wana uhakika wa kumaliza juu ya msimamo ni pamoja na;

1. Mamelodi Sundown

2. Wydad Casablanca

3. Esperance De Tunis

Hivi ni Vigogo au Miamba ya kiafrika ambapo sote tunafahamu kuwa USHINDI kwao ni lazima. Iwe jua au iwe mvua.

Kwa upande wa Simba, inafahamika kuwa hawapo katika ubora wao ambao unafanana na ule wa akina Miqquisone. Hata kufuzu kwao ni kwa sababu walipata fursa ya kuwekwa katika kundi jepesi lenye timu dhaifu kama Horoya AC na Vipers SC.

Ipi nafasi ya washiriki hawa wenye matumaini ya kufika nusu fainali na wakijua kabisa team yao sio ya ushindani kama walivyo wenzao Yanga SC?

View attachment 2561747
Nani kashinda goli Bora la wiki?
 
Yanga walivyowajinga wamempigia kura mchezaji wa al ahly.
 
Washindi wa makundi mengine ambao wana uhakika wa kumaliza juu ya msimamo ni pamoja na;
1. Mamelodi Sundown 2. Wydad Casablanca 3. Esperance De Tunis
Hivi ni Vigogo au Miamba ya kiafrika
na hao vigogo wote uliowataja wanacheza Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), sio shirikisho
🤣
🤣 🤣
 
Ona wanavyomtukana mpayukaji wao na takwimu zake za kujitengenezea
da014118026c4b6d867a2de4ead9e92a.jpg
 
Back
Top Bottom