John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel amekiri kuwa ana hofu kuwa kuna uwezekano wa wachezaji ambao wanaelekea kumaliza mkataba klabuni hapo wanaweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Hatua hiyo inakuja baada ya mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich kutangaza mpango wake wa kutaka kuiuza klabu hiyo.
Abramovich amefikia maamuzi hayo baada ya presha kuwa kubwa kwake kutokana na urafiki wake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye taifa lake linaishambulia Ukraine kijeshi.
Baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao inaelekea ukingoni ni nahodha Cesar Azpilicueta, Antonio Rudiger na Andreas Christensen.
“Huwezi jua maamuzi hayo (klabu kuuzwa) inawezekana yanaweza kuwa na matokeo chanya au hasi,” anasema kocha huyo.
Source: Daily Mail