Baada ya Chirwa kugoma kurudi, Mkwasa afunguka

Baada ya Chirwa kugoma kurudi, Mkwasa afunguka

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Uongozi wa Klabu ya Yanga, umekiri kwamba kuna wachezaji wengi wa timu yao bado wanaidai klabu hiyo fedha za usajili akiwemo Mzambia, Obrey Chirwa ambaye hivi sasa yupo kwao.

Imeelezwa kuwa, Chirwa aliyejiunga na Yanga msimu uliopita, amegoma kurejea kikosini hapo ambapo hivi sasa yupo akifanya shughuli zake binafsi huku akishinikiza kulipwa stahiki zake ili arejee kuitumikia timu hiyo.

Licha ya kutowekwa hadharani Chirwa na wenzake wanaidai Yanga kiasi gani cha fedha, lakini Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amemuomba Mzambia huyo kurejea kuendelea kuitumikia timu huku taratibu za kulipwa zikiendelea.

“Ni kweli kuna wachezaji wengi wanaidai klabu fedha za usajili akiwemo Chirwa, lakini kugoma kurudi si suluhisho, anatakiwa arejee aweze kuitumikia timu huku tukiangalia namna ya kumlipa stahiki zake.

“Ni fedha za usajili tu lakini masuala mengine wanapatiwa kila kitu kama bonsai za mechi na mishahara, lakini anapokaa nje ya timu anaiathiri timu, unaweza kuona kama mechi iliyopita dhidi ya Mbao tumepoteza pointi kitu ambacho hatuwezi tena kufanya kuzirudisha.

“Hali ya uchumi hivi sasa imebadilika, alitakiwa awepo kikosini stahiki zake atapata tu hatuwezi kumnyima,” alisema Mkwasa.

Chanzo: Salehe Jembe
 
Ooooh Manji, oooh Manji njoo okoa jahazi. Siku hizi hata za kununua mechi hamna. Nawaonea huruma watani zangu, ila Mungu atawapambania.
 
Yaani hadi yanga wanadaiwa pesa za usajili?
 
Mlitusumbua sana kununua match. Acha twende sawia tuone IPI ni timu bora hapa tz
 
Ooooh Manji, oooh Manji njoo okoa jahazi. Siku hizi hata za kununua mechi hamna. Nawaonea huruma watani zangu, ila Mungu atawapambania.
Ohoooo Ohoooooo MO Ohoooooo Ohoooooo MO. Ni vilabu vyote vikuu vinategemea wafadhili. Sio yanga tu. Na Simba nayo.
 
BILLY ISISWE,uwezi kuongelea Yanga bila kuitaja Simba!!
 
Back
Top Bottom