Baada ya Corona ni kuinua uchumi wa nchi

Baada ya Corona ni kuinua uchumi wa nchi

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
207
Reaction score
677
BAADA YA CORONA NI KUINUA UCHUMI WA NCHI.

Leo 13:15pm 24/03/2020

Ikitokea moto halafu ukazimwa utabaki Moshi na muda si mrefu Moshi utaisha na hali ya hewa itarudi kama kawaida,Corona imepita umebaki moshi wake nao utaisha, Nini kinafuata? Changamoto mpya ya kuinua Uchumi wa nchi ndio kitu kinachofuata.

Kwa kasi ya Ajabu, Watanzania wameitikia wito wa kunawa mikono kwa Sabuni, Kampeni ya usafi duniani kote haijapata kutokea. Mara hii kwenye maduka na migahawa, unakutana na ndoo za maji ya kunawa kwa sabuni, tuendelee na Utamaduni huu siku zote ili huyu kirusi corona hasipate nafasi tena.

Si hapo tu ukienda kwenye vituo vya mabasi,ukienda ofisini,ukienda bar hata hotelini,Umma unashiriki kwenye mapambano dhidi ya Corona,kwa hakika tumeishinda corona,tuendelee kufanya kazi kwa bidii tuipeleke Tanzania kwenye Uchumi wa kati.

Nakubaliana na kila anayesema tuwazuie watokao kwenye nchi zilizo na maambukizi makubwa lakini sio kufunga mipaka, maana kufunga mipaka ni kurudisha uchumi wetu miaka mitano nyuma,

Nchi yetu ifikirie kuzuia wasafiri kutoka kwenye nchi zilizo kwenye rangi nyekundu kimaambukizi wasiingie nchini mwetu. Ndugu zangu, Wenye kutushauri tufunge mipaka yetu nahofia wanataka ‘ Kutuingiza chakani’ kiuchumi.

Nimemsikiliza Kiongozi wa Chadema akitaka tufunge mipaka,nimueleze tu tumepata kuwa na gonjwa hatari la kipindupindu miaka ya 1970 hadi 1980 tuliweka kalantini mitaani lakini hatukufunga mipaka.

-Kipindupindu cha 1976-1980 hatukufunga mipaka.

Corona haiambukizi kama cholera/kipindupindu watu kati ya 1976 _1980 mlikuwa bado wadogo au tulikuwa hatujazaliwa.

Kipindupindu kililipuka na kuua watu wengi sana,Karantini iliwekwa kwenye mitaa na kazi ziliendelea kama kawaida kuweza kuijenga nchi na Uchumi wake.

Ukitaarifiwa kwa simu ya kukoroga kuwa mtaa wenu umewekwa karantini unawaaga wenzako kuwa mtaonana karantini ikiondolewa! huku wengine wakiendelea kuchapa kazi kama kawaida wala mipaka haikufungwa.

Cholera ulikuwa ugonjwa wa aibu kwa vile kupitia chakula utakuwa amekula kinyesi! Na ukianza kuharisha mpaka unakata roho! Marehemu walikuwa wanazikwa na watu wasiozidi watano!

Baada ya mazishi waombolezaji wengi walipata kipindupindu na kufariki dunia! Ndipo lilipokuja suluhisho ya kuchemsha maji,ikawa tabia tulioizoea ya kuchemsha maji ili kujikinga na kipindupindu na baadae maji ya kuchemsha yakatusaidia kuepukana na typhoid!

Kama sasa ukikohoa kidogo utajihisi corona lakini wakati huo ukiumwa kidogo tumbo la kuendesha unajishuku labda tayari kipindupindu!Tofauti haja ya mtu cholera ilikuwa rangi ya maji yaliyooshewa mchele! Sasa kama sio kipindupindu ukicheki ni rangi ya kawaida unashukuru kuwa sio muuaji kipindupindu!

Sasa kwa hili la Corona hatujafikia huko, na tafsiri ya kufunga mipaka ina maana ya kujifungia na kupunguza shughuli za kiuchumi. Madhara yake ni makubwa mno.

Kwanini tujiingize huko wakati tayari tunazijua nchi zenye maambukizi makubwa na wagonjwa wengi pia. Ni kuwazuia wasafiri kutoka nchi hizo wasiingie nchini. Ni nchi kama Italia, Hispania, Uholanzi, UK na Ubelgiji.Katika Jiji la Wuhan nchini China kwa sasa maambukizi hakuna tena, hii ni tafsiri kuwa tunaweza kupambana na corona kwa kudumisha usafi na kufuata maagizo yote ya Wizara ya afya na tukaishinda corona bila kuathiri shughuli za kiuchumi katika nchi.

Ndugu zangu Watanzania tuwekeze katika suluhu za afya ambazo zinaweza kusaidia katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa corona sasa na baadae, Wakati huo huo kusaidia katika kujiandaa kwa ajili ya kuwekeza katika jamii kwa siku za usoni.

Athari za ugonjwa wa corona ni pamoja na kushuka kwa shughuli za kiuchumi,tuendelee kufanya kazi kwa bidii ili kudhibiti hali ya baadae ya kuporomoka kiuchumi, Nchi yetu Tanzania imezungukwa na nchi nyingi majirani ambao tunategemeana kiuchumi,kila siku wazambia 50,Wamalawi,Wazimbabwe,Msumbiji,Wakongo utawaona Kariakoo na bandari ya Dar es Salaam wakichukua bidhaa na magari yao waliyoagiza toka Japan.

Uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa kasi katika siku za karibuni na kufikia wastani wa asilimia 6 mpaka asilimia 7.Hakuna nchi yoyote nyingine Afrika Mashariki iliyoweza kukua kwa kasi hii na kwa muda mrefu hivi, Tanzania imekuwa kipenzi cha uwekezaji, utalii na biashara kutokana na mazingira mazuri tuliyonayo,tusirudi nyuma kusimamisha shughuli za kiuchumi kwa sababu ya Ugonjwa.

Tuendelee kuupiga vita ugonjwa wa corona kwa kuosha mikono kila wakati, kutumia tishu au kitambaa tunapokohoa, tuepuke kugusa uso kwa mikono kabla ya kunawa.

Tuchukue hatua ya kwenda hospitali tunapoona dalili za koo kuwasha, kukosa pumzi nenda hospitali kamuone daktari kujua afya yako.

Unapohisi homa kali joto kupanda,kukohoa, kuwa na tatizo la kupumua, kuumwa na misuli chukua hatua za kwenda kwa daktari.

Virusi vya corona, vinaweza kusababisha mtu uugue na wengi watu wenye shida ya mapafu.Virusi vya corona bado havijapata kinga, unaweza kupata tena corona haijalishi kama uliugua mwanzo au la, kwa mujibu wa Shirika la afya duniani,uwezekano wa kupatikana chanjo ya corona ni kabla ya miezi 18,

Shime watanzania tuache hofu na tupige kazi kwa bidii tuijenge nchi yetu ya Tanzania.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Unafananisha kipindupindu na Corona?Kweli akili zenu ni sawa na za Nzi wa chooni!
Wakati huo huo wao wamekimbia jiji,wako Dodoma wanapunga upepo juu ya mawe!
 
Umeandika ndeeeeefu, embu summarize kwanza maana ulichoandika hakivutii kukisoma. Kwa ufupi unaonyesha kutoelewa vizuri kuhusu huo ugonjwa, unazungumzia uchumi upi wakati hata nchi zenye uchumi mkubwa duniani zinangamia kwa COVID-19 ? Tahadhari ni bora zaidi kwa sababu huu ugonjwa haukingwi wala kutibiwa kwa uchumi, kwahiyo tukiwa bize kutaka kukuza uchumi, tunaweza kuangamia woteee.
 
Back
Top Bottom