Baada ya Dr. Slaa kufunua nyongeza; Sheria ya "mbwembwe" ni batili?

Watanzania tumepatikana haswa, Nchi imefanywa kama kichwa cha Mwendawazimu. Tushirikishane ili Tuamue moja, kuondoa wote wanaoturudisha nyuma kupitia uchaguzi ujao. Ni maamuzi tu, Nia Ipo, Uwezo Upo, sasa tunashindwa nini?
 
Rais yupi ? huyu mzee wa Bagamoyo,
kama uvumi kuwa bwana mkubwa kaoa wake wengine wawili tangu aingie Ikulu magogoni ni kweli hakika hawezi kuwa na muda wakuwaza matatizo ya WaTz ama kusoma nyaraka zenye kurasa nyingi na kufanya uchambuzi makini.
nasema haya kwasababu kibinadamu kama kweli anawake watatu anahitaji kupata muda wa kutosha kuweza kuwakeep busy, kuwapa haki yao ya ndoa kwa zamu, na kisha anahitaji kwenda kwenye mabembea Jamaika, anahitaji kwenda kupimwa akili kule west Indies, huo muda atapata waapi.
huyu ni rais ambaye kuutwa anahudhulia sherehe za unyago na Jando kule Bagamoyo ama kwenda kula pilau la kwenye hitima mitaani .
muda wakupitia makabrasha atapata waapi ?
kweli kwa mwenendo wa Rais huyu Taifa limekula hasara.
 
Ikiwa Muungwana anapelekewa document bila kusona na anaanguka mkono iko siku atapelekewa document ya kuuzwa kwa nchiyake na akaanguka huku akitabasamu....

Atafura na kufurika lakini hakuna hatua yoyote ile itakayochukuliwa hiyo ni DANGANYA TOTO TU!
 

i cant believe this rumor, yaani kama ni kweli basi bongo hatuna raisi, aliwezaje kusaini doc ambayo hajaisoma, kama ni hivo basi hiyo doc irudishwe na kusainiwa upya, make sasa itatumikaje wakati ni doc haramu--------hiyo sio sheria tena.
 
i cant believe this rumor, yaani kama ni kweli basi bongo hatuna raisi, aliwezaje kusaini doc ambayo hajaisoma, kama ni hivo basi hiyo doc irudishwe na kusainiwa upya, make sasa itatumikaje wakati ni doc haramu--------hiyo sio sheria tena.
ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni bin Bagamoyo.....endeleeni kushangaa.
 
Kila kitu kinachohusu sheria hiyo kilichofanyika baada ya kuisaini , ni batili; hata kanuni ni batili!
Welldone Dr. Slaa!
 
Udhaifu wa viongoz wanao sinzia. Mwanasheria mkuu angenikuta mim hana kaz 24hr.
 
Jamani nipeni shule. JK ana kosa gani? kweli mnataka rais achukue ORIGINOL (iliyopelekwa bungeni) kisha alinganishe na anaotaka kusaini (mpya)!!! come on naona tunazidi kumlaumu sasa.

Prezidaa ana wasaidizi kibao wa kuweza kufanya kazi hiyo.

Mnyonge mnyongeeni ila haki yake mpeni
 

Mbona Dr Slaa kasoma na kagundua kasoro?

Hao akina January Makamba et el wanafanya nini kama si kukagua hii kazi?

Walipomdanganya kwenye daraja la Msummbiji aliwafanya nini?
Wamemdanganya kwenye Maralia no more, amewafanya nini?
Walipomdanganya kwenye ambulance, kawafanya nini?

Yeye si ndiye BOSS wao? Ukiona jinga fulani linakudanganya kila siku, dawa ni kumfukuza kazi palepale. Watakaofuata wataanza kuweka heshima. Kwa sasa inaonekana timu nzima wamemfanya Babu/nyanya wa kuchezea.

Sisi hatuwafahamu hao wasaidizi zake. Kikatiba ni yeye anayewachagua na anaweza kuchagua hata Sokwe mtu. Yes, kwani katiba inamruhusu. Ila Sokwe mtu likiboronga, atakejibu ni yeye. Ingelikuwa ni bunge linamchagulia, basi ni bunge tungekula nalo sahani moja. Ndiyo maana UOZO wa baraza zima la Mawaziri hadi Waziri Mkuu, ni yeye anabeba lawama. Kama wangelibadili katiba na Bunge lichague PM na Rais apitishie na baadaye PM achague mawaziri wake, kesi nyingi zingelipungua kwa Kikwete na kwenda kwa PM. Na nafikiri PM na Rais pangelikuwa hapatoshi. Ila sasa hivi, mambo poa kabisa. PM na Mawaziri, wote wakimuona Rais wanaufyata. Na kibaya zaidi ni kuwa Waziri anaweza kuwa na sauti zaidi ya PM, kwani si wote wamewekwa na Rais?
 
wadau mimi nilikuwa sijasoma gazeti la Tanzania Daima, kweli hii ishu imetokea, lakini sioni kama kweli raisi alikuwa halijui hili, maana yake ni kwamba yeye hajui kama kwenye bunge hicho kipengele hakikujadiliwa so asingeweza just from no where agundue hilo, kwa mantiki hii mimi namtetea Mr. President, has got nothing wrong done, waliofanya vibaya ni waale kwa makusudi yao binafsi wamepindisha ukweli wa kipengele chenyewe
 

Kila mtu anaweza kuingizwa mjini. Hata mie ninaweza kuingizwa mjini. Ila tofauti ni kuwa kama mie ningelikuwa ni Rais na wewe Kabuche ndiyo msaidizi wangu uliyekuwa ulipitie swala zima, basi ufahamu kuwa au huna kazi au unarudi kufanya kazi za chini kabisaaa ambazo ulikuwa ukifanya zamani. Itabidi nikupe adhabu kali ili iwe ONYO kwa wengine. Sasa yeye kafanya nini hadi leo hii?
 
Sikonge,

Yap tumlaumu kwa kutowachukulia hatua wasaidizi wake na sio kwa kusaini huo muswada
 
Hiyo ni inaitwa system flawau niseme Process Flaw

Na flaw hizi na zipo nyingi kwenye utendaji wa serikali nzima. Hakuna kanuni za kufuatwa kuwa kabla rais kusaidi doc "X" inayohusu mambo ya katiba/teknolojiaa/sheria inatakiwa ipitiwe na kuthibitishwa na mtu mwenye post "Z" kutoka ofisi "K"

SCENARIO INAWEZEKANA IKO HIVI
-Inaezekana wahusika muhimu walipewa copy/ kivuli cha doc kupitia badala ya doc halisi . Then washauri wakamwabia mkuu iko sawa. mhh kumbe doc halisi mhhh.

AU
Chama(CCM) kilipewa jukumu la la mwisho kuicheki kabla Mwenyekiti hajasign. Mhhh

Mambo mengi yanaenda kwa uzoefu. usishangae mtu asiye sahihi kama mchapaji akatolewa kafaraau Mwenye wajibu hasa wa kosa kuhamishwa[/B] ikulu ndogo ya Lindi.

It is a Government System operation flaw sijui kama Utumishi wana power juu wa ya wafanyakazi wa ikulu.

Some one must go lakini JK ajue kuwa hizi flaw ziko serikali nzima na wasanii wanazitumia au na yeye kazitumia huko nyuma bila kujua
 

FP.. kama kweli tatizo ni wasaidizi mbona hakuna aliiyewahi kuwajibishwa hadi hivi sasa? wanasema the "buck stops with the president". Kama watu walioboronga miaka minne chini ya uongozi wake ndio hao hao wanaendelea kuboronga na yeye anajua wanaboronga (case in point suala la cheki, magari, mtumbwi, helikopta, ) kwanini hakuna aliyebadilishwa? Sheria yenyewe siyo ngumu kiasi hicho na haina kurasa nyingine na kutokana na umuhimu wake angejaribu hata kukaa chini na kusikiliza opposite opinion (mimi nilielezea ubaya wake kwenye Star TV na wengine wamefanya kwa njia tofauti).

Tatizo yeye kajizungusha na watu wanaoimba sifa zake na wanaomshangilia kwa vigelegele hana mtu ambaye anamwambia kitu tofauti. Kikuungua ndio tunatakiwa kulalamikia wasaidizi. No sir.. kwa sababu yeye ndiye aliyoipigia debe sheria hii kwa mbwembwe yeye ndiyo ale uchungu wake.
 
Napata shida kuamini kwamba "Muungwana" hakuusika na nyongeza ya kipengele cha 7(3).) Ninukuu kipengere chenyewe:
7(3)For the purposes of subsection (2), "campaign team" means a group of' persons formed by a candidate in the nomination process or a contested election for purpose' of presenting or assisting that candidate in the election campaigns, who have been approved-
(a) in the case of a Presidential candidate, by the Registrar;
(b) in the case of a Member of Parliament, by the District Administrative Secretary; and
(c) in the case of a Councilor, by the Ward Executive Officer.
Source:Election expences Act 2010.

Ukicheck vipengere (a) na (b) ina maana Rais mpaka anasaini halikua hajui kwamba timu yake ya kampeni inatakiwa kupitishwa na Msajili wa vyama? ukija kipengere (b) Ingewezekanaje DAS afanye kazi ya kupitishatisha timu ya kampeni ya mbunge/wabunge wa eneo lake bila Mwenyekiti wa chama husika kutojua(Rais ni mwenyekiti wa chama kimojawapo) Uyo DAS anateuliwa na nani?Hata kama DAS ana WEO wapo chini ya TAMISEMI-je waziri husika wa TAMISEMI anaweza kufanya jambo bila kumuhusisha bosi wake?

Nionavyo hiki kipengele walikiongeza makusudi kupata information za wabunge na wapambe wao ili kuwabana kisiasa. "Muungwana" kuonyesha amefura ni harakati zake kisanii za kujiengua na haibu wakati ni muhusika.Pili siamini kama ofisi ya AG wanaweza kuongeza icho kipengere bila maagizo kutoka juu.Kama amefura AG anasubiri nini kujiengua?
 
Kama umakini umekosekana kwa jambo dogo kama hili basi ile mikataba yenye page kibao inakuaje?? Hii ndio Tanzania yetu wote na Heko Dr. Slaa
 

Haa haaa haaaaa....!!! kaazi kweli kweli! Kwa mtaji huu Rais tunaye... yaani huyu ni sawa na Chifu Mangungo wa msovelo enzi zile za wakoloni! tehe tehee teheee!!
 
Kama umakini umekosekana kwa jambo dogo kama hili basi ile mikataba yenye page kibao inakuaje?? Hii ndio Tanzania yetu wote na Heko Dr. Slaa
This is a very serious issue... Hii sio issue ya umakini, ni issue ya uadilifu... ni nani alichomekea? Kwanini alichomekea? Je sheria ngapi ziliopitishwa na Bunge zimefanyiwa mchezo huu? Nchi nyingine... Mwanasheria mkuu angewajibika na wngine wengi kwenye ofisi yake. Haitoshi kuomba msamaha na kuirudisha sheria Bungeni... Rais angekua ashaitolea tamko... Kikwete government is treating us with no due respect... labda kwasababu haogopi ku loose election tena... eti ni mteule wa Sheikh Yahya na Askofu Kilaini... tutamfanya nini? Nonsense! This is where Tanzanians have made a blunder that 'll dearly cost us for years to come... Mungu ibariki (isamehe) Tanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…