Baada ya Dr. Slaa kufunua nyongeza; Sheria ya "mbwembwe" ni batili?

Baada ya Dr. Slaa kufunua nyongeza; Sheria ya "mbwembwe" ni batili?

Nimependa ulivyoweka habari! Tumezoea wale wenzetu wanakopi gazeti zima na kumwaga hapa! Hivi JMK huwa anamuda wa kusoma anachosign? ama mwenzetu ni ceremonial president?

attachment.php

Hivi hapa walikuwa na maana gani kuandika two hundred wakati figure ni three hundred??? Kweli JK kimeo
 
Dr. Slaa yuko sahii hapa, hawa wakuu wamefanya makosa, hakuna haja ya ku SPIN, badala yake ni kukubali makosa na kurekebisha hiyo sheria. Kikubwa zaidi ni kujifunza ili makosa kama hayo yasifanyike tena huko mbeleni. Ndio maana wenzetu walioendelea, huunda tume ili kugundua kwanini makosa yamefanyika na kisha kuziba mianya ili yasifanyike tena.

Inaudhi unapoona watu wanajaribu ku SPIN hata pale walipokosea, why? Kila mtu anakosea na muhimu ni kujifunza ili kuepuka makosa kama hayo.

Tatizo kuna wakati unaweza ukasema ni "makosa".. lakini wakati mwingine ni uhalifu tu. Hawa watu waliofanya kitendo hicho siyo kwamba walikuwa wanasinzia ni wasomi na wanajua kabisa ni Bunge tu ndiyo lenye haki na wajibu wa kisheria wa kutunga sheria au kuifanyia marekebisho. Hata kufuta neno "may" na kuweka "shall" lazima lipitishwe kwenye bunge! Mtu hawezi kujikalia tu ofisini na kusema jamani tuongeze "nukta" hii kwenye sheria halafu ikawa ni "makosa".

hawa ni wahalifu na kinachotakiwa kufanyika ni kuwatia pingu. Nimesema awali hii sheria ni mbaya hata iliposainiwa kwa mbwembwe. Haya tunayoyaona ni kidogo tu ya yale yaliyoko mbeleni.
 
Tusubiri wabunge wa CCM wamuzomee Slaa au wao hawakuliona hilo,wabunge wa CCM wote hovyo kabisa ,wamejaliwa ukasuku tu,wamekaa kimya kama hawajui kinachoendelea,akina Mwakyembe ambao ndo waliobobea kwenye sheria za katiba wameufyata,hovyooo
 
Kwa nini asaini kitu asichokijua
Naamini alijua alichosaini. Suala hili ni kubwa mno tusivyoweza kufikiri. Ni matumizi mabaya ya madaraka ya kiwango cha hali ya juu.

Hapa kuna mambo mawili. Moja, JK anajiandaa kufanya mbwembwe za kusaini sheria anaacha kusoma sheria kabla ya kuisaini. Narudia, yaani badala ya kufanya maandalizi ya kusaini sheria kwa kuisoma vizuri na kwa makini na kuelewa kilichomo, yeye anafanya maandalizi ya kufanya mbwembwe za kusaini. Kosa hili ni kubwa na hukumu yake ni Bunge kumlazimisha kujiuzuru urais. Pili, ni rahisi kuamini kuwa nyongeza zile zimefanywa makusudi sambamba na juhudi zilizokwisha anza siku nyingi kumfanya JK awe mgombea wa pekee wa chama chake. Kitendo hiki nacho ni kosa kubwa mno na hukumu yake ni Bunge kumlazimisha kujiuzuru urais. Sasa wale wanaomtetea JK wachague moja kati ya hayo mawili niliyoyataja hapo juu.
 
Dk Slaa awashukia Spika Sitta na Werema
Hemed Kivuyo, Arusha - Tanzania Daima
MBUNGE wa Karatu Dk Wilbrod Slaa, amewashukia spika wa bunge, Samuel Sitta na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Warema kuhusu rais kudanganywa katika sheria ya matumizi ya fedha katika uchaguzi.

Kutokana na hali hiyo,amewataka waache kutoa majibu mepesi kwenye hoja nzito tena bila kufanya utafiti.

Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ametaka sheria hiyo irudishwe bungeni katika kikao cha 19 kinachotarajiwa kuanza Aprili ili kifungu ambacho rais Jakaya Kikwete amekisaini bila kujadiliwa bungeni, kiondolewe.

Katika barua yake aliyomwandikia spika wa bunge kulalamikia kauli hizo, Dk Slaa alisema kifungu hicho namba 7(3) cha sheria ya uchaguzi kimemhadaa rais Kikwete na hivyo kwenda kinyume na demokrasia.

"Hivyo,Naomba Serikali ichukue hatua kuwasilisha "miscellaneous Amendment" katika Mkutano wa 19 yaani Bunge la Aprili, ili kifungu hiki ambacho ni kinyume na demokrasia kiondolewe kwenye aheria ambayo rais ameisaini,"inasema sehemu ya taarifa ya Dk Slaa

"Angelikuwa amesoma Mhe. Spika angelikuwa mwangalifu kutamka aliyoyatamka. Mheshimiwa Spika anakiri kulikuwa na mjadala, lakini hakutamka mjadala ulihusu nini, na wala hakumnukuu mwenyekiti wa siku hiyo ambayo alikuwa Mhe. Naibu Spika alitoa maagizo gani.

"Ni hatari kwa viongozi wetu kutoa matamko kwa mambo mazito bila kufanya utafiti angalau mdogo. Mhe. Spika atakubali kuwa kwenye Hansard, hakuna popote ambako imejadiliwa achilia mbali kukubaliwa kuwa timu ya kampeni itathibitishwa na msajili(kwa mgombea urais) au katibu tawala (kwa mgombea ubunge) au na mtendaji wa kata kwa (mgombea udiwani). Hii ni dhana mpya kabisa, siyo tu haijajadiliwa wala haikufikiriwa kama Hansard inavyoonyesha," alisema Dk Slaa.

Alifafanua kilichokuwa kimejadiliwa katika mjadala huo ni hoja ya mbunge wa Bariadi Mashariki Andrew Chenge ambaye alitaka kufanyia mabadiliko hoja ya mabidiliko kuhusu pendekezo la serikali kwamba kifungu cha 7(2) na alitaka makundi ya sanaa yaingizwe baada ya neno "Voters".

"Hivyo ni vyema naye Spika akiri tu kuwa utaratibu wa kutunga
sheria umekiukwa. Haifai kubishana kwa sababu wakati Hansard ndiyo ushahidi wa wazi wa jambo hilo, anaeleza katika barua hiyo.

Dk Slaa anaeleza kwamba anamwona mwungwana mwanasheria mkuu wa serikali kukiri mapungufu hayo, lakini anasikitishwa na kauli yake kwamba anastushwa na kauli ya Dk Slaa.

"Kwanini mwanasheria mkuu aanze kufikiria siasa badala ya kuchukua Hansard,Bill iliyowasilishwa Bungeni, na kuisoma ili kujua kilichoazimiwa na Bunge. Huu ndio utafiti siyo kukurupuka kujibu mambo mazito, hata kama anatumia nafasi yake ili kuficha makosa yake, hali hii haikubaliki katika dunia ya sasa kwa sababu watu ni waelewa.

"Hivyo,Naomba Serikali ichukue hatua kuwasilisha miscellaneous Amendment" katika ,kutano wa 19 yaani Bunge la Aprili, ili kifungu hiki ambacho ni kinyume na demokrasia kiondolewe kwenye Sheria ambayo Rais ameisaini.

Dk Slaa aliyasema hayo huku akionyesha nakala ya barua aliyomtumia Spika wa Bunge, Samuel Sitta akimtahadharisha kuwa makini na matamshi ambayo amekuwa akitoa mara kwa mara bila kufanya utafiti wa kina.

Alisema baadhi ya vyombo vya habari viliwanukuu kwa nyakati tofauti Spika Sitta na Jaji Werema wakisema kuwa hawaamini na hawadhani kama tuhuma hizo zina ukweli na kwamba Dk Slaa anapaswa kuelimishwa zaidi ili kufahamu vifungo hivyo vya sheria ya gharama za uchaguzi na kudai kuwa kauli zao zinakiri na kukataa hivyo kujichanganya .


Nampenda Dr. Slaa. Kwa jiwe moja ameweza kuwaua ndege wengi tu, na bado. Wanasheria wote wanaojidai wamebobea, kimyaa ! Huu usanii wa Mkuu wa Kaya hakika unaambukiza - uwe Spika, Mwanasheria Mkuu, Mbunge, Jaji, Msajili wa Vyama, Mwenyekiti wa NEC, Mkuu wa polisi - kama ni mwanaCCM, umeathirika. Nawahurumia akina Mwakyembe.
 
Kama ni kweli basi ni aibu kupita maelezo.
Sasa wananchi wapime uelewa wa serikali yao juu ya maswala makubwa ya taifa na uzembe wa viongozi wao, atu wanapo sema CCM ya sasa inafanya vitu kwa kukariri wanadai eti ni propaganda wakati ni ukweli mtu , huu uzembe wa kusaini sheria bila kupitia na kuhakiki kile kilchoandikwa na badala yake kukimbilia eti kuweke histori mpya kumbe ni kuweka doa la miaka kwa watanzania ni uzembe mkubwa kwa mamlaka ya juu kupitisha sheria zisizo na mbele wala nyuma, Rais ajiuzulu ama auombe umma radhi vile umma na kumpa SLAA idara ya sheria ikiwa ni chini ya chadema pamoja n bunge la jamuhuri ya muungano
 
Umefika wakati wa kuanzisha post ya kupongeza badala ya kulalamika.

Nampongeza Dr Slaa kwa kazi kubwa anayoifanyia Tanzania ya leo.

Nampongeza Dk Magufuli kwa kuokoa rasilimali zetu. Kesi haiendi kwa sababu Mwanasheria mkuu anaedit sheria za nchi kuipendelea CCM AIBU kubwa.
 
Hiyo picha aliyoshikishwa mfano wa check inachekesha kweli maana ....hela iliandikwa kwa maneno ni tofauti na ilivyo kwa namba!!!!! hata hayo ya kusaini yaweza kuwa kweli maana hao wanao proofread hata hiyo check si walikuwepo!!!!!!?
 
............uliyemteua majuzi tu?
Ndio kwa sababu hana umakini katika kazi yake. Tunataka watu wanaofanya kazi kwa umakini na sii kimazoea. Mkulu serikali imemshinda aondoke tu kistaarabu kuliko kuleta aibu kwa Taifa.
 
Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh! 🙁
 
Mimi namkubali sana Mh. Dr. Slaa kuwa ni mmoja wa Wabunge wachache ambao wanatimiza wajibu wao kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo katika mahojiano yake na mwandishi ameonyesha kutokuwa na ufahamu mzuri wa muundo wa Serikali au ameshindwa kutofautisha nyadhifa za watendaji. Kwenye gazeti la Tanzania daima sehemu ya habari hiyop imesomeka hivi, nukuu:

“Mimi ndiye namwomba Mwanasheria Mkuu, rafiki na ndugu yangu, aisome vizuri kwa kuwa yeye ndiye hajasoma. Amesema vizuri kututaja ambao tulikuwa na mjadala ukumbini, sasa anionyeshe mahali popote katika mjadala huo ni wapi approving authority ilijadiliwa, na kuwa hiyo approving authority iwe Msajili, DAS na WEO."

Halafu sehemu nyingine ikasomeka hivi, nukuu:

"Kwa mujibu wa sheria hiyo, kifungu kidogo cha pili, kinaeleza maana ya timu ya kampeni kuwa ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa zoezi la uteuzi lenye madhumuni ya kumwakilisha au kumsaidia mgombea kwenye kampeni za uchaguzi ambaye amepitishwa kuwania.

“(a) Kwa kesi ya urais watathibitishwa na Msajili, (b) Kwa kesi ya Mbunge watathibishwa na Katibu Tawala wa Wilaya na (c) Kwa kesi ya Diwani watathibitishwa na Katibu Tarafa...,” ilieleza sehemu ya sheria hiyo iliyosainiwa na Rais Kikwete ambayo nakala yake tunayo."


Mh. Dr. Slaa alipojichanganya ni pale alipomwelezea WEO kuwa ni Katibu Tarafa. Usahihi ni kwamba WEO ni kifupi cha Ward Executive Officer ambapo kiswahili chake ni Afisa Mtendaji Kata. Sasa sijui ni yupi ndiye yumo kwenye hicho kipengele kilichochomekwa. Vinginevyo Mh. Dr. Slaa kazi yako nzuri.
 
mimi namkubali sana mh. Dr. Slaa kuwa ni mmoja wa wabunge wachache ambao wanatimiza wajibu wao kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo katika mahojiano yake na mwandishi ameonyesha kutokuwa na ufahamu mzuri wa muundo wa serikali au ameshindwa kutofautisha nyadhifa za watendaji. Kwenye gazeti la tanzania daima sehemu ya habari hiyop imesomeka hivi, nukuu:

“mimi ndiye namwomba mwanasheria mkuu, rafiki na ndugu yangu, aisome vizuri kwa kuwa yeye ndiye hajasoma. Amesema vizuri kututaja ambao tulikuwa na mjadala ukumbini, sasa anionyeshe mahali popote katika mjadala huo ni wapi approving authority ilijadiliwa, na kuwa hiyo approving authority iwe msajili, das na weo."

halafu sehemu nyingine ikasomeka hivi, nukuu:

"kwa mujibu wa sheria hiyo, kifungu kidogo cha pili, kinaeleza maana ya timu ya kampeni kuwa ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa zoezi la uteuzi lenye madhumuni ya kumwakilisha au kumsaidia mgombea kwenye kampeni za uchaguzi ambaye amepitishwa kuwania.

“(a) kwa kesi ya urais watathibitishwa na msajili, (b) kwa kesi ya mbunge watathibishwa na katibu tawala wa wilaya na (c) kwa kesi ya diwani watathibitishwa na katibu tarafa...,” ilieleza sehemu ya sheria hiyo iliyosainiwa na rais kikwete ambayo nakala yake tunayo."


mh. Dr. Slaa alipojichanganya ni pale alipomwelezea weo kuwa ni katibu tarafa. Usahihi ni kwamba weo ni kifupi cha ward executive officer ambapo kiswahili chake ni afisa mtendaji kata. Sasa sijui ni yupi ndiye yumo kwenye hicho kipengele kilichochomekwa. Vinginevyo mh. Dr. Slaa kazi yako nzuri.

kazi ipo kweli kweli!! Aluta kumtimua!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote, maana kama siyo Dr Slaa mambo mengi yalishapita tu hivi hivi

Tangu kwenye Richmond, EPA mpaka kwenye kuchomeka vipengele vya sheria. Cha ajabu Anne Kilango Malechela anatunukiwa na wamarekani nishani ya Mwanamke Jasiri. Mimi ningekuwa na hizo nishani ningemtunuku Dr. Slaa Nishani ya Mbunge Jasiri.
 
Ndio kwa sababu hana umakini katika kazi yake. Tunataka watu wanaofanya kazi kwa umakini na sii kimazoea. Mkulu serikali imemshinda aondoke tu kistaarabu kuliko kuleta aibu kwa Taifa.

Sasa tatizo si aliyemteua....ingawa sishanagai maana kuna DC..Betty Mkwasa nadhani...aliwahi kuteuliwa wilaya mbili tofauti kwa wakati mmoja...
 
Back
Top Bottom