Baada ya Dr. Slaa kufunua nyongeza; Sheria ya "mbwembwe" ni batili?

Nimependa ulivyoweka habari! Tumezoea wale wenzetu wanakopi gazeti zima na kumwaga hapa! Hivi JMK huwa anamuda wa kusoma anachosign? ama mwenzetu ni ceremonial president?


Hivi hapa walikuwa na maana gani kuandika two hundred wakati figure ni three hundred??? Kweli JK kimeo
 

Tatizo kuna wakati unaweza ukasema ni "makosa".. lakini wakati mwingine ni uhalifu tu. Hawa watu waliofanya kitendo hicho siyo kwamba walikuwa wanasinzia ni wasomi na wanajua kabisa ni Bunge tu ndiyo lenye haki na wajibu wa kisheria wa kutunga sheria au kuifanyia marekebisho. Hata kufuta neno "may" na kuweka "shall" lazima lipitishwe kwenye bunge! Mtu hawezi kujikalia tu ofisini na kusema jamani tuongeze "nukta" hii kwenye sheria halafu ikawa ni "makosa".

hawa ni wahalifu na kinachotakiwa kufanyika ni kuwatia pingu. Nimesema awali hii sheria ni mbaya hata iliposainiwa kwa mbwembwe. Haya tunayoyaona ni kidogo tu ya yale yaliyoko mbeleni.
 
Tusubiri wabunge wa CCM wamuzomee Slaa au wao hawakuliona hilo,wabunge wa CCM wote hovyo kabisa ,wamejaliwa ukasuku tu,wamekaa kimya kama hawajui kinachoendelea,akina Mwakyembe ambao ndo waliobobea kwenye sheria za katiba wameufyata,hovyooo
 
Kwa nini asaini kitu asichokijua
Naamini alijua alichosaini. Suala hili ni kubwa mno tusivyoweza kufikiri. Ni matumizi mabaya ya madaraka ya kiwango cha hali ya juu.

Hapa kuna mambo mawili. Moja, JK anajiandaa kufanya mbwembwe za kusaini sheria anaacha kusoma sheria kabla ya kuisaini. Narudia, yaani badala ya kufanya maandalizi ya kusaini sheria kwa kuisoma vizuri na kwa makini na kuelewa kilichomo, yeye anafanya maandalizi ya kufanya mbwembwe za kusaini. Kosa hili ni kubwa na hukumu yake ni Bunge kumlazimisha kujiuzuru urais. Pili, ni rahisi kuamini kuwa nyongeza zile zimefanywa makusudi sambamba na juhudi zilizokwisha anza siku nyingi kumfanya JK awe mgombea wa pekee wa chama chake. Kitendo hiki nacho ni kosa kubwa mno na hukumu yake ni Bunge kumlazimisha kujiuzuru urais. Sasa wale wanaomtetea JK wachague moja kati ya hayo mawili niliyoyataja hapo juu.
 
Dk Slaa awashukia Spika Sitta na Werema
Hemed Kivuyo, Arusha - Tanzania Daima


Nampenda Dr. Slaa. Kwa jiwe moja ameweza kuwaua ndege wengi tu, na bado. Wanasheria wote wanaojidai wamebobea, kimyaa ! Huu usanii wa Mkuu wa Kaya hakika unaambukiza - uwe Spika, Mwanasheria Mkuu, Mbunge, Jaji, Msajili wa Vyama, Mwenyekiti wa NEC, Mkuu wa polisi - kama ni mwanaCCM, umeathirika. Nawahurumia akina Mwakyembe.
 
Kama ni kweli basi ni aibu kupita maelezo.
Sasa wananchi wapime uelewa wa serikali yao juu ya maswala makubwa ya taifa na uzembe wa viongozi wao, atu wanapo sema CCM ya sasa inafanya vitu kwa kukariri wanadai eti ni propaganda wakati ni ukweli mtu , huu uzembe wa kusaini sheria bila kupitia na kuhakiki kile kilchoandikwa na badala yake kukimbilia eti kuweke histori mpya kumbe ni kuweka doa la miaka kwa watanzania ni uzembe mkubwa kwa mamlaka ya juu kupitisha sheria zisizo na mbele wala nyuma, Rais ajiuzulu ama auombe umma radhi vile umma na kumpa SLAA idara ya sheria ikiwa ni chini ya chadema pamoja n bunge la jamuhuri ya muungano
 
Umefika wakati wa kuanzisha post ya kupongeza badala ya kulalamika.

Nampongeza Dr Slaa kwa kazi kubwa anayoifanyia Tanzania ya leo.

Nampongeza Dk Magufuli kwa kuokoa rasilimali zetu. Kesi haiendi kwa sababu Mwanasheria mkuu anaedit sheria za nchi kuipendelea CCM AIBU kubwa.
 
Hiyo picha aliyoshikishwa mfano wa check inachekesha kweli maana ....hela iliandikwa kwa maneno ni tofauti na ilivyo kwa namba!!!!! hata hayo ya kusaini yaweza kuwa kweli maana hao wanao proofread hata hiyo check si walikuwepo!!!!!!?
 
............uliyemteua majuzi tu?
Ndio kwa sababu hana umakini katika kazi yake. Tunataka watu wanaofanya kazi kwa umakini na sii kimazoea. Mkulu serikali imemshinda aondoke tu kistaarabu kuliko kuleta aibu kwa Taifa.
 
Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh! 🙁
 
Mimi namkubali sana Mh. Dr. Slaa kuwa ni mmoja wa Wabunge wachache ambao wanatimiza wajibu wao kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo katika mahojiano yake na mwandishi ameonyesha kutokuwa na ufahamu mzuri wa muundo wa Serikali au ameshindwa kutofautisha nyadhifa za watendaji. Kwenye gazeti la Tanzania daima sehemu ya habari hiyop imesomeka hivi, nukuu:

“Mimi ndiye namwomba Mwanasheria Mkuu, rafiki na ndugu yangu, aisome vizuri kwa kuwa yeye ndiye hajasoma. Amesema vizuri kututaja ambao tulikuwa na mjadala ukumbini, sasa anionyeshe mahali popote katika mjadala huo ni wapi approving authority ilijadiliwa, na kuwa hiyo approving authority iwe Msajili, DAS na WEO."

Halafu sehemu nyingine ikasomeka hivi, nukuu:

"Kwa mujibu wa sheria hiyo, kifungu kidogo cha pili, kinaeleza maana ya timu ya kampeni kuwa ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa zoezi la uteuzi lenye madhumuni ya kumwakilisha au kumsaidia mgombea kwenye kampeni za uchaguzi ambaye amepitishwa kuwania.

“(a) Kwa kesi ya urais watathibitishwa na Msajili, (b) Kwa kesi ya Mbunge watathibishwa na Katibu Tawala wa Wilaya na (c) Kwa kesi ya Diwani watathibitishwa na Katibu Tarafa...,” ilieleza sehemu ya sheria hiyo iliyosainiwa na Rais Kikwete ambayo nakala yake tunayo."


Mh. Dr. Slaa alipojichanganya ni pale alipomwelezea WEO kuwa ni Katibu Tarafa. Usahihi ni kwamba WEO ni kifupi cha Ward Executive Officer ambapo kiswahili chake ni Afisa Mtendaji Kata. Sasa sijui ni yupi ndiye yumo kwenye hicho kipengele kilichochomekwa. Vinginevyo Mh. Dr. Slaa kazi yako nzuri.
 

kazi ipo kweli kweli!! Aluta kumtimua!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote, maana kama siyo Dr Slaa mambo mengi yalishapita tu hivi hivi

Tangu kwenye Richmond, EPA mpaka kwenye kuchomeka vipengele vya sheria. Cha ajabu Anne Kilango Malechela anatunukiwa na wamarekani nishani ya Mwanamke Jasiri. Mimi ningekuwa na hizo nishani ningemtunuku Dr. Slaa Nishani ya Mbunge Jasiri.
 
Ndio kwa sababu hana umakini katika kazi yake. Tunataka watu wanaofanya kazi kwa umakini na sii kimazoea. Mkulu serikali imemshinda aondoke tu kistaarabu kuliko kuleta aibu kwa Taifa.

Sasa tatizo si aliyemteua....ingawa sishanagai maana kuna DC..Betty Mkwasa nadhani...aliwahi kuteuliwa wilaya mbili tofauti kwa wakati mmoja...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…