McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Mchezaji na Nahodha wa zamani wa Klabu ya Manchester United pamoja na timu ya Taifa ya England, Rio Ferdinand, ameweka wazi kuwa atatembelea Tanzania Mei 19 hadi 22, 2026 kufuatia mwaliko maalum kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda.
Kupitia ujumbe wake, Rio amesema amefurahishwa na mazungumzo aliyofanya na Mhe. Makonda pamoja na viongozi wengine kuhusu fursa kubwa zilizopo Tanzania katika michezo, utalii na maendeleo ya vijana.
Aidha, amesema ana hamu ya kujifunza zaidi kuhusu utamaduni wa Tanzania, kukutana na wananchi pamoja na kuona namna ambavyo ushirikiano wa michezo unaweza kufungua fursa mpya kwa vijana wa Kitanzania.
Ziara hiyo inatarajiwa kuwa sehemu ya juhudi za kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia michezo, utalii na diplomasia ya kiuchumi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Source: Kusaga TV