Ndugu yangu,
Nakuita ndugu yangu kwa kuwa u mwanaume mwenzangu. Kwanza pole sana kwa mkasa uliokupata. Najua umeumizwa sana rohoni mwako, lakini kaza moyo, tulia kwanza utafakari. Hata mimi yalinikuta kama yako... lakini BAADA ya kuoa. Sikurudi nyuma... nilisonga mbele, na sijutii. Ukiwa na msimamo, ushikilie.
1. Suala la mimba ni tata. Je, umehakiki kweli kwamba anayo? Mwambie twende kwa daktari, akupime, na huyo daktari awe wako wewe, sio wake, kwani anaweza kuwa amepanga mpango matokeo yawe kwamba ana mimba.
2. Kama ana mimba, mwambie huna imani kwa kuwa alikucheza shere, kwa hiyo mwambie hutatoa matunzo mpaka ithibitishwe kwa njia ya DNA, kwamba mtoto ni wako. Amechezea shilingi ******, sasa apate adabu kidogo. Atalea mimba peke yake.
3. Suala la kurudiana hapo halipo. Umetangaza nia ya kuoa, yeye anakutenda? Kama kweli alikuwa na mapenzi ya dhati kwako, hata angetongozwa namna gani, ASINGEKUBALI! Mwanamke namsifia kwa msimamo wake, AKIPENDA. Akipenda amependa kweli, anaweza hata kufa kwa ajili ya ampendaye. HUYO HAKUKUPENDA! Short and clear!
Sina ushauri zaidi ya haya, ila nakutakia kila la kheri. Utampata wa kwako, aliyetulia, na nakuombea kwa Mola akupe faraja, upate kupona jeraha hilo kubwa ulilolipata.
-> Mwana wa Haki
P.S. Kuvishwa pete ya uchumba ni jambo ambalo wanawake wengi waliofikisha umri wa kuolewa wanalililia. Ni bahati kubwa kwao. Nadhani hapa wote mnanielewa. Huyu kavikwa pete, tena kwa shangwe zote, lakini anafanya mambo ya kihuni! Kaitia aibu familia yake! Nadhani huko kwao watakapojua kilichotokea, anaweza hata kutengwa kwa kuwaaibisha! Jamani, muwe na busara wanawake!