Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,252
- 18,335
Katika siku 100 kwanza za Rais SSH alipata uungwaji mkono mkubwa kutoka makundi mengi kwa muda mfupi. Ilikuwa kama nchi ndo imetoka kupata uhuru kutoka kwa mkoloni. Kumkosoa katika jambo lolote lilikuwa kosa kubwa sana maana ungepewa majina kama Mataga, Sukua gang nk. Ilionekana kama alipata mashabiki wa kufa kupona kwa kipindi kifupi kabisa.
Sasa baada ya mkutano wake na wahariri mambo yameanza kubadilika hasa baada ile kauli yake kuhusu katiba na marufuku ya kufanya siasa kwa vyama vya siasa. Watu wameanza kusogea katika nafasi zao za awali kwa kasi kubwa. Ni kama utamu wa fungate la utawala mpya umeisha hivyo wameanza kuonja ladha halisi ya kile kichokuwa nyuma ya fungate.
Watanzania wanafahamika vizuri wakianza kusakama. Hutowaona barabarani ila maneno yao yatakufikia ulipo na yatakuchachafya kwelikweli. Nadhani hiki kipindi kimeshaanza rasmi.
Ngoja tuone atatumia njia gani kuhimili vishindo; kuacha waongee, kuziba masikio, kuwafunga midomo au kukimbia.
Yetu macho.