Baada ya Gwambina kujitoa Ligi Daraja la Kwanza (Championship), Ndanda nayo yajitoa

Babumawe

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2014
Posts
2,556
Reaction score
2,571
Klabu ya Ndanda ya Mtwara imetangaza kujitoa katika Ligi Daraja la Kwanza (Championship), huku sababu ikielezwa ni ukata kiasi Cha kushindwa kumudu gharama za kujiendesha.

Ndanda imekuwa haifanyia vizuri kwenye ligi hiyo kuanzia mwanzoni na sasa inaonekana kuamua kuachia ngazi rasmi.

Timu hiyo ilipaswa kusafiri kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili mchezo dhidi ya COPCO Veteran katika Uwanja wa Nyamagana lakini walikosa fedha za kugharamia safari hiyo.

Baada ya hali hiyo Uongozi umetangaza kujitoa rasmi kwenye Ligi hiyo huku ukisisitiza walijaribu kuwashirikisha wadau mbalimbali ili wapate msaada lakini ilishindikana.

Ndanda inafikia hatua hiyo ikiwa inashika nafasi ya 15 baada ya kuvuna alama 15 huku ikiwa imesalia michezo mitatu dhidi ya Biashara United, Pan African yote ugenini huku mchezo mmoja dhidi ya Transit Camp ingekuwa nyumbani

Ndanda inakuwa ni timu ya pili msimu huu kujitoa katika Ligi Daraja la Kwanza (Championship) baada timu ya Gwambina kufanya hivyo katikati ya Msimu wa Ligi.

Ikumbukwe Gwambina ilijitoa kwenye ligi hiyo ikiwa mzunguko wa kwanza unaelekea ukingoni kwa madai ya kuonewa kila wakati na mamlaka ya soka nchini.
 
Dah pole yao
 
Huko sio kwa yule Mkuu wa Mkoa aliyeahidi kutoa Milion kwa kila goli kwa ile timu ya Kariakoo?
 
Yaani serikali ya mkoa imeshindwa kuinusuru team yetu,??
Ni aibu, wana DC, wafanyabiashara, mbunge wao, wapenda soka. Wangepitisha harambee kwenye chakula cha usiku mmoja,wangepata ya kumalizia ligi.
 
Back
Top Bottom