Baada ya haya nani anastahili kuwajibishwa

Baada ya haya nani anastahili kuwajibishwa

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
2,944
Reaction score
2,032
Ninaandika kwa mwandiko wa machozi mengi baada ya kushuhudia kilichotokea Bukoba ziwani namna tulivyoshughulika kuokoa watanzania wenzetu na hata wengine kupelekea kupoteza maisha Sitaki kujikita sana huko maana tuko siku nyengine mpya. Je hii inchi yetu. Imekosa kweli vifaa vya uokaji?

Mpaka watu binafsi waje watoe kama, wananchi watoe nguvu zao kuvuta ndege au kijana mmoja ajitoe muhanga kupambania maisha ya wengine? KODI ZETU WATANZANIA. Je azitoshi kununua vifaa vya uokaji vikawepo kila mkoa, Mbona kodi zetu zinanunua Magari mengi ya kifahari kwa viongozi Mbona kodi zetu zinatumika sana kuwasafirisha Viongozi kwenda nje kuomba mikopo, kwanini tangu ajari za mv spice Mv bukoba mbona kodi zetu hazitumiki kwenda nje kuomba vifaa vya uokozi?

Mv Spice, MV Bukoba hadi leo tumepata majanga ya ndege wahusika wanaotutawala hamjajifunza jambo au ni makusudi.

Ninawaomba Viongozi wetu kwa msemo huu wa wahenga ukitaka kula na kipofu usimshike mkono,

Kupitia ajari hii nilijua kuna watu wangekuwa tayari kwa kuona aibu wangejiuzuru lakini hamna hilo hadi muda huu. Basi nyie mlogoma kujiuzuru tokeni mbele endesheni kampeni za kututaka watanzania tuchangie vifaa vya uokozi muhimu kila mkoa tupo tayari kupitia TOZO.

Kuliko kuona bado tuko kwenye zama za watu binafsi kujitolea kama,kujitolea kuogelea,kujitolea majeneza, kujitolea kama.WABUNGE MKO WAPI KUITAKA SEREKALI ITOE TAMKO LA KUNUNU Helcpter za UOKOZI Watanzania tumechoka viongozi wa michongo.
 
Hakuna wa kuwajibishwa. Ndiyo imeisha hiyo!

Nani ajiuzulu, ili aanze kukaa foleni barabarani kama sisi makabwela!!
 
Nchi ya majuha hii hata wafe watu wa mkoa mzima wadanganyika wataona sawa tu wala hawatawashinikiza viongozi kujiuzulu
 
Tusha sahau aya mbona kama kawaida yetu Watanzania. Move on
 
HAKUNA wa KUWAJIBIKA ZAIDI ya kupandishwa Vyeo utashangaa mkuu Wa ZIMA MOTO Kagera akawa wa KANDA
 
Back
Top Bottom