Matango
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 535
- 118
Wakuu habari za leo,
Naomba radhi kwa watakaoelewa tofauti na nilivyoelewa mimi. Niwashirikishe katika maswali niliyoulizwa na Babu mmoja jana kwenye kituo cha daladala ambacho kina pilikapilika nyingi za biashara kwenye jiji la kiuchumi la DSM.
Nilifika kwenye meza yake ya biashara ya matunda kutaka kupata huduma nikakuta mjadala siyo mkali lakini mzito wenyewe wanaongea taratibu kama vile hawataki mtu mwingine awasikie.
Nilipofika mimi nikajaribu kuchangia, walikuwa wanaongelea mikutano ya vyama vya siasa. Nikamwambia yule Babu kwani kuna tatizo? Mbona mikutano imeruhusiwa na imeshaanza?
Hapo nikachokoza Mzinga wa nyuki au sijui Bomu la Ukraine. Yule Babu akapiga swali moja mzinga kuelekea kwangu, Akasema:, "Sikiliza Bwanamdogo, mimi hapa nafungua biashara yangu na hata huyu bibi hapa unayemuona anauza chakula, mimi nafungua kila siku saa 9 alasiri, huyu bibi anakuja saa 12 jioni, tunafanya hizi biashara mpaka saa 6 usiku na wateja wapo kwa wingi tu.
Sasa nakuuliza wewe unayeshabikia mikutano ya hadhara, mkienda kule kwenye mikutano kuanzia sijui saa ngapi... hadi saa 12 jioni inafungwa, mnapata kitu gani ? kama hujafanyakazi mchana ukaacha chochote kitu nyumbani, hiyo familia yako ukirudi unawaletea nini?
Au mimi nikiacha hiyo siku biashara yangu nikaenda kusikiliza hizo hotuba nitapata nini? Ninavyokumbuka siku za nyuma wakimaliza mikutano ya hadhara tunaambiwa kesho ni siku ya kupiga kura. Sasa safari hii wakimaliza hiyo mikutano yao ya mfululizo, tunaenda kupiga kura wapi?.
Nikamwambia Babu ! Babu ! Una maswali magumu ? Tuwaachie wenye siasa zao. Nipatie tu mzigo wangu wa embe nipeleke nyumbani kwa watoto.