Baada ya interview 'Shuu Salon' nashauri DNA iwe lazima pale mtoto anapozaliwa. Cheti cha kuzaliwa kiambatanishwe na cha DNA

Baada ya interview 'Shuu Salon' nashauri DNA iwe lazima pale mtoto anapozaliwa. Cheti cha kuzaliwa kiambatanishwe na cha DNA

Hii interview ya huyu dada anayeitwa Shuu Salun mmeiangalia?

Yaani huyu dada alicheat, alafu akaja kumwambia kaka wa watu kuwa hiyo mimba ni ya kwake na alisema ALIPANGA kabisa kupata hiyo mimba na mchepuko wake

Mimi naona tukija na huu mfumo itasaidia kupunguza tata au shaka kuhusu nani baba halisi wa mtoto na itapunguza Paternity Fraud kwa 90%

Yaani hakuna mtoto kupewa cheti cha kuzaliwa bila kupimwa DNA

Faida za Kufanya DNA Wakati wa Kuzaliwa​

  • Kuzuia Migogoro ya Uzazi: Inaondoa utata au shaka kuhusu nani baba halisi wa mtoto tangu siku ya kwanza, jambo linaloweza kuzuia migogoro ya kifamilia na kisheria huko mbeleni.
  • Kuzuia Mchanganyiko wa Watoto: Inasaidia kuhakikisha mtoto habadilishwi hospitalini—iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi.
  • Ulinzi na Utambulisho (Security): Kama mtoto akipotea, akitekwa, au ikitokea maafa, taarifa zake za DNA kwenye mfumo wa taifa zinasaidia kumtambua kwa haraka na kwa usahihi wa 100%.
  • Afya ya Mtoto: Vipimo vya kigenetiki vinaweza kusaidia kubaini mapema hatari ya magonjwa ya kirithi na kumwezesha daktari kutoa matibabu sahihi mapema.



Angalia anavyojibu bila hata haya kabsa!
Hebu tufike pahala zitungwe sheria za kijinai kuhusu mambo ya mahusiano! Women have become too devilish!
 
Sio tu kupima DNA bali pia na itungwe sheria kali ya kuwaadhibu wanawake watakaobainika kuwafanyia ulaghai wanaume baada ya matokeo ya DNA.....

Napendekeza adhabu iwe jela miaka kumi na faini ya gharama zote alizotumia mwanamume kwa kipindi chote alichokuwa akihudumia mimba mpaka mtoto akidhania ni wa kwake
 
Mkuu, dawa za Malaria tu bado tunapewa msaada, kununua mashine za kupimia DNA nchi nzima tutaweza? Kipimo cha DNA hakifanyiki kama cha Malaria,mashine zake zinazohitajika ni za gharama kubwa, hatuwezi kumudu hilo kwa sasa, huo ndo uhalisia.
Na pia gharama za kupima DNA nani atalipia? Kuna watu hata kulipia tu gharama ya kujifungua hawawezi,gharama za DNA ndo wataweza? Labda kama kiwe kwa wenye uwezo na serikali iwe tayari imemudu kununua hizo mashine za gharama za DNA.
 
Tabia hii ni mbovu kuna binti mmoja yupo kama mbili kasoro sababu ya kubarishiwa baba kila mwaka.
 
Mkuu, dawa za Malaria tu bado tunapewa msaada, kununua mashine za kupimia DNA nchi nzima tutaweza? Kipimo cha DNA hakifanyiki kama cha Malaria,mashine zake zinazohitajika ni za gharama kubwa, hatuwezi kumudu hilo kwa sasa, huo ndo uhalisia.
Na pia gharama za kupima DNA nani atalipia? Kuna watu hata kulipia tu gharama ya kujifungua hawawezi,gharama za DNA ndo wataweza? Labda kama kiwe kwa wenye uwezo na serikali iwe tayari imemudu kununua hizo mashine za gharama za DNA.
Tunaweza ishu ni vipaumbele tu. Bajeti inayotumika kununua magari ya viongozi tu kila mwaka inatosha kabisa.
 
Back
Top Bottom