Kama tulivyo sikia siku ya Alhamis, raia wa jimbo la Catalonya wapiga kula ya kujitenga na Uhispania, sababu ziko nyingi.
Vuguvugu hili lilianzishwa na viongozi wa jimbo hilo akiwemo rais wa jimbo hilo Charles Puigdemont.
Viongozi wa juu wa Uhispania ametupilia mbali matokeo ya kura hiyo ya maoni na kutishia kuufutilia mbali uongozi mzima wa jimbo hilo pamoja na jimbo hilo kuongozwa directly from Madrid.
Waziri mkuu wa Uhispania, Mariano Rajoy amelitaka bunge la Senate la Uhispania kuidhinisha hatua hiyo na kuitisha uchaguzi wa jimbo hilo hapo Desemba 21 mwaka huu.
Kwa EA, nchi yenye utawala wa majimbo ni Kenya, baada ya sintofahamu ya uchaguzi wa marudio wa Kenya, baadhi ya Wabunge wa upinzani walitishia kuitisha mswada wa majimbo yao kujitenga na Kenya huku wakidai katiba yao inawaruhusu.
Kinachoshangaza zaidi, Kenya ina majimbo 47 lakini majimbo 4 yaliyotishia kujitenga hadi leo hayajafanya uchaguzi kutokana na vurugu za hapa na pale.
Je, kwa jinsi tulivyoona nguvu ya upinzani wa Kenya basi kama hili litakuwa agenda yao basi huenda majimbo ya magharibi mwa Kenya, Migori, Kisumu, HOMABAY na Isiaya ikiwemo na mkoa wa pwani wa mombasa zikafuata mkondo wa Jimbo la Katalonya ya Uhispania.