pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 282
- 561
Salaam Aleykum ndugu katika imani,
Nilisikiliza hii kauli ya mheshimiwa RC Dar Chalamila ikabidi kwanza nitafute hao uduvi wanaoongelewa hapa ni kitu gani, nikagundua uduvi ni dagaa wa kamba wale wadogo wenye mimba mingi.
Nikatembea kwa wauzaji wawili watu nikagundua waujazi uduvi huwa hawauzi uduvi pekee bali wanauza pweza, ngisi kachori na huo uduvi, binafsi ni mpenzi sana wa pweza na nikienda kwenye meza ya pweza naacha zaidi ya shilingi elfu tatu.
Nadiriki kusema meza moja inayouza pweza, ngisi kachori na hao uduvi anauhakika wa kulaza zaidi ya elfu hamsini.. ukitoa gharama za uendeshaji huyu mtu kwa mwezi anauhakika wa kupata zaidi ya shilingi laki tano ni mshahara mkubwa kuliko mtumishi anayeanza na TGS yaani Tanzania government scale pia ni mshahara mkubwa kuliko hata teller wa bank.
Ukweli ni kwamba hizi sekta zisizo rasmi zina kipato kingi kuliko ajira rasmi ambapo makato yanakaribia nusu ya mshahara hivyo wauza uduvi tuendelee kupiga kazi kuna siku Mungu atatuona.