Tetesi: Baada ya kelele za wabunge wa upinzani, Rais akubali kupandisha mishahara ya watumishi wa umma. Kutangazwa rasmi 04-05-2019

Tetesi: Baada ya kelele za wabunge wa upinzani, Rais akubali kupandisha mishahara ya watumishi wa umma. Kutangazwa rasmi 04-05-2019

Ukweli nikuwa hata akipandisha hali ya uchumi ni mbaya, atapandisha tu ili kupunguza kelele na miradi mingi itadorora kwani mingi ilifanyika kusaka sifa za kisiasa na sio uwezo halisi wa serikali. Sioni Magufuli akifanya mradi mwingine wa maana awamu yake ya pili, kwani hafanyi vizuri kama alivyotaka kutuaminisha na uwezo wake kiuchumi unazidi kudhihiri kwamba ni mdogo.
 
Kama ni kweli waziri wa utumishi pamoja wabunge wote CCM wasiongezwe hata mia.wamezidi uoga.

Mimi kuna wakati naona bora awepo Magufuli na wabunge wa upinzani tu.nchi ingeenda vizuri.maana wabunge wa upinzani ndiyo wanaomshauri raisi.wabunge wote wa ccm naonaga hawajielewagi hata wanatetei maslahi ya nani

kidogo sana Mh.Bashe na Nape ndiyo wabunge pekee kidogo naonaga wajitambua

Ndiyo maana naona hata Magufuli anaamuaga kujifanyia mambo yake hata nje ya bajeti.kwa sababu wabunge wanaopitisha hiyo miipango ya hovyo ndiyo hao hao CCM.bajeti ambazo wapinzani huwaga wanazikataa wao wanazipitisha.Ndiyo maana hata mkuu wa Nchi anazitupaga kapuni
 
Back
Top Bottom