Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Habari Wanajamvi,
Baada ya kelele za Wananchi wa Mwanagati, Ilala, Dar es Salaam kuhusu ubovu wa barabara yao na kusababisha hadi nauli ya daladala kupanda huku magari yakiwa yanaharibika, sasa imeanza kufanyiwa kazi.
Soma: Hali ya Barabara kwa Wakazi wa Mwanagati inasikitisha
Jana Desemba 21, 203 grader limepita na kusawazisha barabara hiyo kuhakikisha walau inapitika kwa urahisi na kuleta ahueni kwa Wananchi hao waliolalamika barabara hiyo kwa muda mrefu sana.
Pamoja na hayo pia barabara hiyo ambayo pia ipo katika Jimbo la Ukonga la Mbunge na Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa imeanza kuwekewa lami ambapo tayari kipande kidogo kimewekewa lami huku Mkandarasi akiwa anaendelea na kazi
MY TAKE:
Wananchi tusiache kupiga kelele kwa tatizo lolote tunaloliona Viongozi wanapita humu na wanaona kila kitu.