Baada ya kifo cha Ruge Mutahaba (RIP)ndipo tunaona Joe Kusaga ni kama ‘anajitambulisha’ pale Clouds Media, je ni kweli alikuwa ‘amefunikwa’?

Baada ya kifo cha Ruge Mutahaba (RIP)ndipo tunaona Joe Kusaga ni kama ‘anajitambulisha’ pale Clouds Media, je ni kweli alikuwa ‘amefunikwa’?

Na Ruge hakua CEO pale clouds.
Kwenye kampuni yeyote kuna CEO na Owner.

Ni mara chache ukakuta CEO ni Owner.

Na ni mara chache zaidi kukuta Owner anafahamika zaidi ya CEO wa hiyo kampuni.

Kusaga alikuwa mmiliki na Ruge alikuwa anasimamia shughuli za Clouds za kila siku.

Mawazo yanaweza yakawa ya wote wawili ila kwasababu Ruge ndo anayasimamia ataonekana 'genious' tu.
 
Nini kimebadilika katika hayo, ni vipi sasa anataka kufahamika?
Sasa amechukua majukumu ya kuwa CEO.

Ndio maana kila siku mnamsikia. Ila mwanzoni alikuwa kimya zaidi ya sasa.
 
Umepuyanga private company CEO ndio owner kuna cheo kinaitwa COO cheo cha COO ndicho kinaweza mfunika CEO
Sio wakati wote.

Makampuni mengi binafsi yameajiri CEO na shareholders wamekaa pembeni.
 
Umepuyanga private company CEO ndio owner kuna cheo kinaitwa COO cheo cha COO ndicho kinaweza mfunika CEO
Wewe ndo umepuyanga vibaya mno.
Si lazima CEO awe ndo mmiliki wa kampuni. Tena kwa kampuni kubwa kabisa mmiliki anajitoa kuwa CEO anabaki kuwa chairman nyie mnapambana uko kwenye vikao. Microsoft na Google wamiliki wake wapo lakini sio ma-CEO. Hata Bakhresa sio.
 
Umepuyanga private company CEO ndio owner kuna cheo kinaitwa COO cheo cha COO ndicho kinaweza mfunika CEO
wewe ndiyo zero kabisa...kampuni yoyote inayojielewa CEO hawezi kuwa ndio owner..
 
Simba mwenda pole ndiyo mla nyama. Ruge kaendaaa! ghafla bin vuup! bila kutegemea kapambana na Mysterious power!!! Nguvu hii imemaliza out of public and his willing!!

hata kwenye familia hawakosagi vihere here! kwenye maziko, misiba. sherehe!!! ndo wanalogwaga kwanza, wakati tego siyo lao! mlengwa anakuja bidaye sana, wakati walozi wakesha kata tamaa na uganguzi juzi! Ruge alitumika kama antenae ya Radar!
 
Amestukia kutrend kunalipa, anataka akifa azikwe kwa shangwe zote kama Ruge
 
Wewe ndo umepuyanga vibaya mno.
Si lazima CEO awe ndo mmiliki wa kampuni. Tena kwa kampuni kubwa kabisa mmiliki anajitoa kuwa CEO anabaki kuwa chairman nyie mnapambana uko kwenye vikao. Microsoft na Google wamiliki wake wapo lakini sio ma-CEO. Hata Bakhresa sio.
Mkuu naona wewe ndio kama umepiyanga.

Jamaa yupo sahihi ila umemissinterpret hapo kwenye 'lazima' jamaa hajasema lazima ilo neno umeweka wewe.

Kitakwimu private company CEO wengi ndio wanakuwa Owner kwamaana ya Owner ni yule mwenye share nyingi...fanya study yako kampuni kubwa za silicon valley.
 
Sasa nilichokosea kipo wapi. Nilisema "si lazima CEO awe owner". Uongo kwani?

Yeye alisema "private companies CEO ndo owner". Ni sahihi?

Mimi sijakataa CEO kuwa owner ndo maana nikaweka "si lazima", nadhani tafsiri yake unaielewa. Yeye hajaweka conditions, kasema as if hakuna kinyume na msimamo wake.
 
Inaoneka Clouds wamekosa muongoza njia, Kusaga anajaribu kujaza hiyo nafasi bila ya yeye mwenyewe kuijua njia.

Ngoja tuone ubunifu wao wa vipindi utakwendaje, maana tangu Ruge aondoke sijasikia lolote jipya au lenye bashasha zaidi ya vijana wao kuonyesha nia ya kutaka kuikimbia Clouds, kuelekea stations zingine au CCM.

Hapo ndo tutaamini maneno ya Ruge, kuwa kile ulichonacho ndani yako, kichwani na moyoni, talanta yako, ni yako mwenyewe. Hakuna wakuigelezea ikampa matokea yale yale inayokupatia wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom