Baada ya kipigo, Kocha wa Yanga akubali muziki wa Simba

Baada ya kipigo, Kocha wa Yanga akubali muziki wa Simba

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amekisifu kikosi cha klabu ya Simba na kusema Wachezaji wa Yanga walikosa ubunifu ndio maana wamepoteza mchezo wa jana

Zahera amesema ushindi wa jana wa Simba dhidi ya timu yake unakuja wakati ambapo klabu hiyo ya Msimbazi ingeshinda tu maana kwa sasa inacheza vizuri

Amesema timu yake ina Wachezaji wazuri lakini wanakosa ubunifu ule wa utafuta suluhisho la namna ya kucheza na kufunga magoli tofauti na ilivyo kwa Wachezaji wa Simba wenye uwezo huo

Hata hivyo amesisitiza kuwa bado Simba inafungika kirahisi sana na msimu ujao timu yake ya Yanga itamfunga Simba

Soma pia; Ligi Kuu Tanzania Bara, Februari 16, 2019: Kariakoo Derby, Yanga SC 0 - 1 Simba SC - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aende tu Kazi imemshinda huyu mamluki
We kweli kocha wa yanga unaisifia simba? Huyu sio huyu kabisa tena hatuna utamaduni huo kabisa
 
Zahera ni mwimbaji wa mipasho2 hana lolote yanga mpelekeni akashiriki uko kwenye SAUTI ZA BUSARA

Sent using Jamii Forums mobile app


Safari hii Yanga wamepatikana, walisema huyo ndiyo kocha anayewaambia ukweli wa Tanzania, atasaidia sana maendeleo ya mpira sasa kawaambia Simba alistahili ushindi. Sikumbuki Kocha yeyote wa Yanga kwa kumbukumbu zangu kuwahi kusema hivyo.
 
Back
Top Bottom