Baada ya kipigo toka kwa Fury, Wilder atemana na kocha wake. Asema alivalishwa mavazi mazito, miguu ilichoka

KITAULO

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Posts
1,926
Reaction score
2,797
Bondia Mmarekani Deontay Wilder ameamua kutemana na mkufunzi wake au mwalimu wake (Kocha) Mark Breland baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Muingereza Tyson Fury.


Kupitia ukurasa wa Twitter wa Boxing Kingdom umeripoti kutokea kwa taarifa hizo.

Hii imekuja baada ya mwalimu huyo wa muda mrefu kurusha taulo uwanjani ili kumtaka mwamuzi asitishe pambano hilo kwenye raundi ya 7 ambapo ilionekana Wilder kuzidiwa na mwisho wa pamabno hilo Wilder alipoteza ubingwa wa WBC kwa TKO dhidi ya Tyson Fury.

Mbali na hilo , imeelezwa Wilder amejieleza kwamba mavazi yake ambayo aliyavaa wakati akiingia ulingoni usiku ule wa pambano lake dhidi ya Tyson Fury ndio chanzo cha kupoteza pambano hilo. Amesema vazi lile lilikuwa na uzito wa Kilo 18, hivyo lilichosha miguu yake na kupelekea kupokea kichapo hicho kwa TKO.


“Hakuniumiza hata kidogo, lakini ukweli rahisi ni kwamba sare zangu ndio zilikuwa nzito sana kwangu,” Wilder alimwambia Yahoo Sports. “Sikuwa na nguvu miguuni tangu mwanzoni mwa pambano. Katika mzunguko wa tatu, miguu yangu ilipigwa kama na butwa hivi. Lakini mimi ni shujaa na watu wanajua kuwa mimi ni shujaa. ”


“Watu wengi walikuwa wakiniambia: ‘inaonekana kana kwamba kuna kitu hakipo sawa kwako’ lakini kumbe kweli, lakini wakati upo jukwaani unatakiwa kusahau kila kitu, Nilijaribu sana kufanya kila jambo lakini Nilijua fika sikuwa na nguvu miguuni kwa sababu ya sare zangu, ” – Maneno ya Wilder
 

Attachments

  • 1582636586177.png
    291.9 KB · Views: 1
Alisema even God cannot assist Furry to win, leo tena anasema Nguo nzito, ukweli ni kwamba jamaa alishazidiwa sana sikio lilivimba sana likawa kama kiazi ni hatari kuendelea namna ile kwani Nguo nzito alivalishwa si angezikataa alipokua anapewa kwanza nguo zile zimejaa matangazo ina maana ni hela kapiga nyingi kwa kuvaaa kama kamtimua kocha basi hana shukrani.

Mzee alitupa taulo kumsaidia. Kwa round ile na alivyokua amejeruhiwa angeweza kuwa kiziwi milele. Alipigwa kinoma noma.
 
Halafu hizo costume zilikuwa kilo ngapi sasa...eti 18kg...mchezaji wa heavy weight alichoshwa na hizo kilo...shubamiti...
Mim mwenyewe nilikuwaga na Mazoez ya kawaida, napiga jumla ya weight kama 12kg. Napiga mbio mdo mdo, ankle weight kilo 4, na juu kifuani nane. Hapo sijabeba kitu mkonon wala wala back pack.

Nalikuwa na mudu fresh tu. Sasa mzee hapo 18kg kwa heavyweight, kakwama mzee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akubali tu kwamba amepigwa tu ajipange tu kwa kipindi kingine il afanye vizuri
 
Kama sio mbeleko ya refa na kasi ndogo ya Fury, Wilder alikuwa anakaa raundi ya tatu. Kuna combo alipigwa raundi ya tatu mpaka Wilder mtandao wake wa miguu ukayumba kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…