Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Bila shaka yoyote ile sasa ni dhahiri kwamba Ben Saanane alikwishauawa kikatili, na ni dhahiri kwamba Maiti yake ilitupwa (Rejea Kitabu kinachouzwa kwa kasi cha shujaa Kabendera)
Ninaamini kwenye dini zote upo utaratibu wa kuwazika kiroho Marehemu ambao wamethibitika kufariki lakini Miili yao haikupatikana, kwa maana ya kufa kwa ajali ya moto ama kuliwa na Mamba au hata majanga mengine yanayoweza kusababisha mwili wa marehemu kutopatikana.
Ndio Maana nimeuliza ni lini Chadema pamoja na Familia ya Marehemu Ben Saanane itaitisha kusanyiko kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho za hayati huyo ambaye sasa imethibitika kwamba Hatunaye.
Namuomba Mwenyezi Mungu aipokee Roho yake, Amina.