Baada ya kivuko kupata changamoto, mitumbwi yatumika kuvuka Kigamboni

Baada ya kivuko kupata changamoto, mitumbwi yatumika kuvuka Kigamboni

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Baada ya kivuko kupata changamoto, wasajiriamali wamejiongeza, huu ndio usafiri wa dharura huko Kigamboni kwa ambao wanaona darajani ni mbali. Mitano tena

IMG_1925.jpeg
 
Usafiri hatarishi sana huu.

Abiria Hawana lifejackets na chombo kimeoverload. Mcheki jamaa wa nyuma karibia anagusa maji.

Serikali inataka utokee ajali ndiyo wapoge marufuku. Si wampe Bahresa kazi kama wao wameshindwa asee?
Uyo bakharesa ndiye anaehujumu Uchumi wanaharibu kwa makusudi ili wajukuu zake waingize vivuko wapige pesa. Usalama wa Taifa wamebaki kuuza mahindi tu.
 
Mitumbwi imeua sana watu late 80s na mwanzoni mwa miaka ya 90 mpaka walivyoletewa MV Usiwe Kupe au MV Dezo.....Badala ya kwenda mbele wanarudi nyuma.
 
Hivi hapo wameshindwa kabisa kujenga daraja la juu, au hata la kufunga na kufungua?

Naona kama kule Kurasini ni mbali sana na mjini.

Kulikuwa na umuhimu gani wa kujenga daraja la Tanzanite kabla ya Magogoni?

Sure ,wamefanya mambo hayana mantiki.

Daraja la Tanzanite ni useless ,lilikuwa halina priority ilitakiwa lijengwe baada ya kukamilisha madaraja ya umuhimu.

Daraja la nyerere halijasaidia chochote ni sawa na kuzunguka Kongowe kuja kigamboni tu,nalo lilikuwa halinza ulazima.

Wachina wameadvance sana kwenye madaraja ya kufunga na kufunguka ,wajenge pale lebanoni to Kigamboni.
 
Baada ya kivuko kupata changamoto, wasajiriamali wamejiongeza, huu ndio usafiri wa dharura huko Kigamboni kwa ambao wanaona darajani ni mbali. Mitano tena

View attachment 3021406
Hiyo mitumbwi siwezi kupanda hata kidogo.

Ile boti tu ya Azam naiogopa sembuse hiyo mitumbwi 🤣🤣🤣🤣🤣🤣.

Wakazi wa huko wanapata tabu sana.
 
Back
Top Bottom