Baada ya kuagiza Pizza kwa miaka 10, ghafla kuna kitu hakikuenda sawa!

Baada ya kuagiza Pizza kwa miaka 10, ghafla kuna kitu hakikuenda sawa!

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Ilikuwa ni mwaka 2020, anajulikana kama Alexander Kirk alikuwa ni mmoja wa wateja kindaki ndaki wa Pizza katika Duka la Domino.

Majirani wanasema ni mtu ambaye ni mara chache kuonekana mtaani na hata alipokuwa anagongewa mlango basi ilikuwa ni mara chache sana kuitikia au kufungua mlango.

Lakini pamoja na Tabia yake hiyo majirani hawakujua kwamba alikuwa na ukaribu sana na wasambazaji wa Pizza kutoka Domino store, huko ndiko alikokuwa ana agiza Pizza online kila siku iendayo Kwa Mungu kwa muda WA miaka 10 mfululizo Bila kukosa.

Ilikuwa kawaida Sana Kwa staff wa Domino store kila siku jioni kupokea oda toka kwa mteja wao mwaminifu na hivyo kukawa na bond kubwa Sana kati ya Alexander na wale staff, maana sasa walikuwa kama ndugu, maana kipindi cha Miaka Kumi (10) sio mchezo lazima walijenga mahusiano mazuri Sana Kati ya mteja na staff wa Domino store.

Ila kuna kitu hakikuenda Sawa ambacho kiliwashangaza staff wa lile Duka la Pizza. Zilikuwa zimepita siku Kumi na moja (11) tangu mteja wao Alexander alipoagiza Pizza Kwa mara ya mwisho.

Bilashaka hata kama ingekuwa wewe lazima ingekushangaza kidogo, inakuwaje mteja ambaye kwa kipindi cha Miaka 10 mfululizo anaagiza bidhaa toka katika Duka lako halafu mara ghafla tu haonekani unashangaa kakata mguu, kama kweli unamjali mteja wako lazima utakuwa na hamu ya kujua je kuna tatizo gani?

Basi wale staff wakashauriana Kwanza kwenda nyumbani Kwa Alexander, walipo fika waligonga mlango na kuita Sana lkn hawakuitikiwa, lakini Kwa mbali wanasikia sauti ya television na taa zinawakaa,hii iliwashangaza Sana. Wakarudi store kwao na kumpa habar meneja wao.

Lakini bado kuna kitu kilikuwa kinawasumbua bado, hapo awali walijua labda mteja wao huenda alisafiri na kwenda nje ya mji wake,lkn kile kitendo cha kukuta taa zinawaka na television IPO on kana kwamba kuna mtu mule ndani,hiyo haikukaa Sawa katika vichwa vyao,walipata na machale au guts katika nyoyo zao.

Hapo wakaona wapige 911 kutaka msaada zaidi kwasababu kuna kitu kinawaambia mambo hayapo Sawa, na kweli walipiga 911 opareta akapokea na kumtaarifu kuwa mteja wao ambaye alikuwa na kawaida ya kuagiza bidhaa kutoka kwao lkn mara ghafla hakuagiza tena na walipo mtembelea nyumbani kwake kuna mazingira ambayo yanawapa mashaka kidogo.

Basi kweli wakaja polisi na paramedics tayari kwa kukabiliana na chochote ambacho watakutana nacho,Kwa mara nyingine waligonga tena na Kwa mbali wakasikia sauti ya mtu ambaye anaomba msaada,ndipo wakavunja mlango na kumkuta Alexander yupo Chini sakafuni,wale watu WA ambulance walichukua chap na kwenda nae hospital.

Iligundulika kwamba Alexander ana historia ya kupata stroke ndogo ndogo na hata walipo mkuta siku Ile alikuwa amepata stroke, na Madaktari wanasema kwamba Lau kwamba ingepita siku moja zaidi basi huenda wangempoteza Alexander, shukrani Sana Kwa staff wa Domino Kwa kuamini guts/ machale Yao kwamba kuna kitu hakikuwa Sawa na kuchukua hatua kumfuatilia mteja wao.

Baadae meneja WA branch Ile bwana Fuller pamoja na assistant meneja wake walialikwa katika kipindi cha Good morning America, walisema ni kawaida yao kuwa karibu na wateja wao na kuwa sehemu ya familia yao na hiyo sio mara ya Kwanza kutoa au kusaidia wateja wao mara wanapo pata changamoto mbali mbali. Host wa kipindi aliwapongeza Sana Kwa kuamini Ile sauti yao ya ndani kwamba kuna kitu hakikuwa Sawa kuhusiana na mteja wao.

Ni hayo Tu!

Ijumaa Mubaraka.
1676009628860.jpg
 
Back
Top Bottom