Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Hiyo hewa ya ukaa inapimwaje?

Watalaamu wanakuja shambani kwako,wanapima ukubwa wa shamba lako,kisha wanagawa shamba ktk plots za kuchukua sample, kisha kila plot wanapima kipenyo cha miti kadhaa,wanachukua umri wa miti husika,kutokana na formula yao wanapata biomass ya miti yako, kutokana na biomass hiyo wanapata uzito wa carbon iliyonyonywa na miti yako. Bei kwa tani moja mi sijui,ila nilishiriki zoezi la kupima mahali fulani.
 
Umuhimu wa kufahamu kufahamu Kiwango cha hewa ya ukaa shambani kwakiu ni upi?
 
Umuhimu wa kufahamu kufahamu Kiwango cha hewa ya ukaa shambani kwakiu ni upi?

Sasa hawa jamaa wakishapima hiyo hewa ya Ukaa na wakapata kiwango ulicho nacho, wanaandaa report ya shamba lako na kuipeleka ofisi ya makamu wa Rais. Sasa pale ofisi ya Makamu wa kuna fungu ambalo unatakiwa uchotewe kila mwaka kwa sababu miti yako inasafisha anga. Baadhi ya vijiji tayari vimeingia ktk mpango huu, hasa ktk utunzaji wa misitu asili.

Walio anza mapema hii kitu wameshalipwa, hasa Makampuni, nimeshuhudia kwa green resources limited iliyopo Iringa. Kwa sisi individuals ndio inaanza. Malipo yatakuwa yanatolewa kila mwaka kwa kadri mti unavyokuwa. Ukikata miti yako ndio mwisho wa allowance, kwa sababu kila wakati wanaweza kuona shamba lako kama bado lina miti au la.
 
Aisee malila hiyo ni Dili sana. Nitakutafuta kwa maelezo zaidi.
 

Mradi kujiendesha mwenyewe ni faida tosha kiongozi .... nafurahi tumekuwa wengi tulonufaika na JF na ujasiliamali;
 
Aisee malila hiyo ni Dili sana. Nitakutafuta kwa maelezo zaidi.

Huu mradi ukiweza kuingia na serikali wakamaanisha,watu wataotesha miti kama vichaa,maana hela yake ni ndefu balaa.
 
Hongera sana mkuu.. na mimi nilikua nataka kujua heka ni sh. ngapi huko na zinapatikana kiurahisi? Pili nilikua natakja kujua kuku singida uliwapata wapi? nina banda langu hapa nyumbani, nahitaji kuku wa kufuga lakini mimi sio mwenyeji singida. unaweza nipa maelekezo zaidi jinsi ya kufika huko singida vijijini?
 

Mnaotaka mashamba nawashauri tuwasiliane. Msije mkaenda kununua kwenye hifadhi. Niliweka namba hapo tuwasiliane. Pia Kama unataka kuanza na kuku wachache ni bora ukaenda kuwafata sokoni hapo ulipo. Mimi nilipanga nianze na kuku 100. Yule mwenyeji niliyomtanguliza akaninunulie kuku alipofika huko kwao akaanza kutumia pesa yangu kwa bia. Nilipokwenda ilinipasa niingie mwenyewe mtaani ndipo nilipotoka na hao 30. Pia piga mahesabu ya nauli. Pia huko singida kuna msimu ambao kuku hupatikana kwa bei poa. Hasa kipindi cha njaa hapo utakuwa Kama unawaokoto vile. January , February , March and April wako cheap.
 

Malila kweli we ni kiboko, tena nashawishika kusema we ni PhD holder. Nways asante kwa kunifumbua macho kaka. Natumaini project yangu ikisimama itabidi uje unitembelee. Ama kweli JF ni chuo kikuu...
 
Mungu awe mlinzi wenu siku zote Malila na mleta uzi awape maisha marefu ili mzidi kutuelimisha. Kwa kweli michango yenu imenipa hari na msisimko wa kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji.mkuu ebarhad next year if God wishes nItakusumbua sana kwani nilishapanga kuja kuwekeza huko. So usinichoke mkuu pindi nitakapoanza kukusumbua kuanzia kupata ardhi na mengineyo.Mkuu malila wewe ni zaidi ya phd una moyo wa kipekee, Mungu awe nawe siku zote.
 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru kwa kutuombea baraka. Be blessed. Tupo Pamoja kwa kadri Muumba wa vyote atakavyotuwezesha. Mungu ni mwema.
 

Mrembo,pole na majukumu.
Nimeona kwenye post yako umepanda miti ya Mitiki Pwani. Mie nina eneo Rufiji ,je Mitiki inakubali huku?
 
Mrembo,pole na majukumu.
Nimeona kwenye post yako umepanda miti ya Mitiki Pwani. Mie nina eneo Rufiji ,je Mitiki inakubali huku?

kwakweli mi sio mtaalam wa maeneo, ila najia mitiki inastawi maeneo yenye joto kiasi na mvua at least mara 2 kwa mwaka. nnavosikia sehemu kubwa ja ukanda wa pwani inastawi vizuri tu.

Labda wataalamu Malila wanaweza toa msaada zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa shule hiyo. Ntazidi kutafuta ufahamu wa zao hili.Hii ni pension bakubwa.
 
kwakweli mi sio mtaalam wa maeneo, ila najia mitiki inastawi maeneo yenye joto kiasi na mvua at least mara 2 kwa mwaka. nnavosikia sehemu kubwa ja ukanda wa pwani inastawi vizuri tu.

Labda wataalamu Malila wanaweza toa msaada zaidi.

Rufiji kwa ujumla mitiki inamea vizuri, kuanzia Kibiti,Muhoro mpaka Somanga, Mitiki inamea vizuri. Kaza buti uoteshe mingi. Wilaya ya Kisarawe na baadhi ya maeneo ya Mkuranga/Bagamoyo mitiki inagoma sana. Sababu kubwa ni mvua na udongo.
 
nimesikia wivu sana na hongera mno...umenitia moyo sasa nitaaza rasmi baada ya hii shule kwisha:smile-big:
Malila ubarikiwe sana kwa miongozo yako bila hiyana nimejifunza mengi kupitia hili jukwaa

pamoja sana
 
Last edited by a moderator:

Dahh... mbarikiwe sana Malila na mwanzisha uzi, huu uzi ni muhimu sana, yani kila siku lazima niupitie kama mwanafunzi anayejiandaa na mtihani vile, coz naamini na mimi ni mfanyakazi ninaye jiandaa kujiajiri.

Nina maswali machache mkuu, kuna shamba tunamiliki huko Kondoa, lina ekari 150, limepimwa na lina documents zote muhimu, huwa tunalima alizeti, lakini lina miti mingi sana tuliyoikuta wakati tunalinunua na hatuna mapango wa kuikata, nimevutiwa sana mpango huu wa hewa ya ukaa. Je kwa kupitia shamba letu hilo, nasi tukitaka kuanza kuitafuna hiyo keki ya hewa ya ukaa, inabidi tufate hatua zipi? Yani tunaanzia wapi kufatilia, pili kuna gharama zote za wali zinazotakiwa?

Thanks....
 

Nipe e mail yako kwa pm ili nikuunganishe na jamaa wa SUA ili wakupe majibu ya mahitaji yako moja kwa moja.
 
nimesikia wivu sana na hongera mno...umenitia moyo sasa nitaaza rasmi baada ya hii shule kwisha:smile-big:
Malila ubarikiwe sana kwa miongozo yako bila hiyana nimejifunza mengi kupitia hili jukwaa

pamoja sana

Ameen.Baraka ziwe kwetu sote.
 
Usijali mkuu. Nitakupm ili tuwasiliame. Tena kwa yeyote atayetaka mitiki nitamuunganishia miche Kwa sh 300 Kwa mche. Kipindi kipindi Cha kupanda mitiki ni kipindi Cha mvua.

Mwakashina mlongo!
Aisee, nitakupigia unipe maujanja, nimekuatamanije! Hongera sana kwa kazi nzuri, napenda sana ufugaji wa kuku, ila nilipokuaj mjini nikastop kwasasasa naanza tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…