Ni carbon dioxide,
Kwenye respiration ya miti,kuna wakati mti huhitaji oxygen na baadae hutoa carbon dioxide ambayo tena huchukuliwa na mimea hiyo hiyo na mwisho hutoa oxygen.
Kilichotokea duniani ni kwamba hewa ya carbon dioxide imezidi sana(shughuli za viwanda), kiasi kwamba mimea iliyopo haiwezi kufyonza yote, hata maji hayawezi kufyonza, hata udongo hauwezi kufyonza kuimaliza nk. Kwa hiyo wenye dunia wamekuja na mpango wa kuongeza miti zaidi ( mkataba wa kyoto) duniani. Nchi zote zenye viwanda vingi pamoja na makampuni yenye viwanda yanachangia mfuko huu.
Kwa hiyo mtu ye yote aliyeotesha miti baada ya mwaka 1990, yaani baada ya Mkataba wa Kyoto anastahili kulipwa posho kwa sababu miti yake inapunguza hewa hiyo. Kwa hapa Tz SUA ndio wanashughulikia suala hilo.
Watalaamu hawa wa SUA, wanapima kipenyo cha mti,wanachukua umri wa mti,kupitia formula yao wanapata Biomass, kutokana na Biomass hiyo wanapata uzito wa hewa hiyo kwa tani. Bei kwa tani moja ni siri mkuu.Kuna makampuni kadhaa ya misitu wameanza kulamba malipo, ni malipo manene kaka.
Nimekupa kwa ufupi sana,ili walau ujue
kinachoendelea.