Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hongera sana umefanya kitu cha maana mi nilianza na kuku 13 sasa hivi ni mwezi wa nane toka nianze nina kuku 92 ambao baada ya miezi 2 wataanza kutaga, pia nina vifaranga 46, na mradi sasa hivi unajiendesha wenyewe ingawa bado sijaanza kupata faida. Hongera sana
laki tano kwa hekaMkuu mashamba huko yamefika bei gan?
laki tano kwa heka
What does you mean?Update mheshimiwa
Aisee mimi mwenyewe nlikua naingia jamii forum kwaajili ya kuangalia Ideas hasa za ujasilia mali...na ule uzi ulikua msaada mkubwa sana kwangu,nmejenga mabanda lushoto na nmeweka Nguruwe nane kwa kuanzia...napenda sana vjana tukipeana njia za kujikomboa wenyewe...Shukrani sana kwa aliye leta ule uzi na wanajamii forum wote walochangia...maana mawazo yao yanasaidia wengi...(nlijua n mm2,kumbe na wengine...!!!!!).Baada ya kumaliza degree yangu ya pili na kuona kuwa ajira kama ajira haiwezi kuwa mkombozi wangu kiuchumi niliamua nifatilie mawazo mbalimbali ya ujasiriamali. Nikafikiria ujasiriamali wa kiubunifu wa hali ya juu ndiyo utakuwa mkomnozi wangu kiuchumi. Nimeanza Kwa kununua shamba lenye ukubwa wa hekari 12 nje kidogo ya mji wa Morogoro ( Kwamakunganya-majichumvu). Sehemu kubwa ya shamba langu nimepanda mitiki.
Baada ya kufatilia humu nikagundua kuwa mradi wa nguruwe na kuku wanalipa sana. Ninaomba kukili kwamba miongoni mwa post ambayo serious nilihaidi kuifanyia kazi ni Anza hivi mpwa wangu. Kwa kuwa imani yangu inaniruhusu nikaona ni laziima niifanya hii ya Anza hivi mpwa wangu. Hivyo nikaanza maandalizi ya kufuga nguruwe na kuku pia. Hivyo nilianza Kwa kuanzia kuchimba na kujengea tangi la maji chini. Ilichukua Muda wa miezi miwili tangu langu la maji kukamilika. Tangi langu la maji Lina uweze wa kujaza maji lita 30 elfu.
Baada ya hapo nikaanza maandalizi ya ujenzi wa banda la nguruwe na la kuku. Baada ya mabanda yangu kukamiliaka nilisafiri hadi singida kufata kuku. Bei ya kuku singida inalidhisha sana. Ili upate kuku wa bei rahisi inakupasa uende vijijini ambako kuku huuzwa cheap. Hivyo nilisafiri hadi kijijini ambako nililinunua kuku 31 ambao ndiyo nimeanza nao.. Kwa upande wa nguruwe nimeanza na 12 ambao niliwanunua wakiwa na miezi mitano. Pia nimeweka kanga na mbuzi Kwa ushauri wa marafiki.
Ninashukuru Mungu ninaanza kuwaona kuku wameanza kutaga Kwa fujo. Pia ninamshukuru Mungu Kwa kuwa ninaona ninaanza kuwa muajili pole pole. Pia ninamshukuru Mungu ninaona mawazo ya kunyanyasika( kuajiliwa) yanaanza kupotea taratibu.Kwa sasa nguruwe wangu wameshabeba mimba hivyo nategemea kuanza kuona mabanda yangu yakijaa vitoto vya nguruwe hivi punde.
Kupitia uzi wangu huu nitakuwa nawataarifu maendeleo ya mifugo yangu Kama sehemu ya kuwatia moyo wajasiriamali wenzangu. Morogoro ni sehemu ambayo wajasiriamali mnaweza kutimiza ndoto zenu Kwa kuwa Ardhi inapatikana Kwa bei nafuu na ni Karibu na Dar kwenye soko kubwa la bidhaa mbalimbali.
vipi feedback Mopalmo ?I must put this into use,and will bring feedback,i promise
vipi feedback Mopalmo ?
eberhard alishafulia, project ilifeli na ndiomaana yupo kimya mpaka leo. Kila akiulizwa hana cha kujibu anaona aibu kwakuwa alikuja kwa mbwembwe afu amechemsha.
Nilimtembelea shambani kwake kiukweli hali ni mbaya ameuza kila kitu amebakiwa na robo eka tu ya shamba ambapo kuna kijumba chake cha kuishi.
Usijali mkuu, katika maisha kufeli ni kawaida na wala usione aibu.