Baada ya kuangalia mechi kadhaa za Niyonzima akiwa Simba

barafuyamoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
32,378
Reaction score
29,739
Habarini!

Mimi ni mshabiki wa Simba Sports Club, ningependa kwemda moja kwa moja kwenye mada kuwa uongozi wa Simba kwa kweli walikurupuka kumsajili Niyonzima. Mpaka sasa kwa kweli sijaona mpira wowote akicheza kuisaidia Simba. Wanamuita pass master ila pasi zake ni sideways zaidi ya forwards.

Ni ukweli usiopingika kuwa Niyonzima alisajiliwa kwa shinikizo la kuvutia tu mashabiki wa Simba kuwa wanachukua mchezaji wa Yanga ambaye kwa misimu kadhaa alikuwa mchezaji wao bora.

Kibaya zaidi kinaniumiza ni Niyonzima (mrwanda) kaja waharibia namba za kudumu watanzania (Ndemla na Mzamiru) ambao kwa kweli walikuwa wanaanza kuchipuka!
Mzamiru na Ndemla wa Simba ni wazuri mara nne ya Niyonzima wa Simba.
Inasikitisha sana, nimekuwa nampa muda ila kwa kweli haoneshi kiwango kipya chochote, pia hakuhitajika Simba maana nafasi zake zilikiwa zina watu tayari wanazitendea haki.

Matokeo ya leo nimeyapokea kwa moyo mkunjufu, kama ni kuweka mkeka kwa kweli niliiona droo ni wiki sasa!
 
Niyonzima ni mchezaji mzuri sana na amekua na kiwango bora kwa misimu kadhaa hivi sasa, zigo la lawama unazompa nazifananisha na mchezaji Paul Pogba wa man utd! Nachokiona mm anacheza kufuata maelekezo ya mwalimu na si vinginevyo, suala la kiwango chake kama ww ni mfuatiliaji mzuri wa soka nadhani hupaswi kuwa na cha kushangaa hapo
 
Niyonzima ni mzuri sana. Mi nadhani kocha ndo bado hampangii majukumu katika nafasi ya kuonesha cheche zake vizuri
 
Unatudanganya wewe ni mshabiki was yanga unania tu ya kumchafua Niyonzima, hivi kunamchezaji simba wa kumlinganisha na niyonzima huyo simba imelamba Dume acha utani
 
Simlaumu, ila ukweli unabaki kama wewe ni mdau wa soka mzuri, hakuhitajika Simba. Vinginevyo ni kwamba unapenda tu kuona mchezaji wa Yanga yegemezi alichukuliwa Simba.
 
Unatudanganya wewe ni mshabiki was yanga unania tu ya kumchafua Niyonzima, hivi kunamchezaji simba wa kumlinganisha na niyonzima huyo simba imelamba Dume acha utani
Sijaona alichofanya mpaka sasa!
 
Twende sawa! Tangu lini usajili wa bongo ukamwachaga mtu salama niyonzima ameondoka kwa kubeza na simba wakamsajili kwa kutukomoa Ila vuteni subra!
 
Simlaumu, ila ukweli unabaki kama wewe ni mdau wa soka mzuri, hakuhitajika Simba. Vinginevyo ni kwamba unapenda tu kuona mchezaji wa Yanga yegemezi alichukuliwa Simba.
Hapana boss! Nafikiri alihitajika kwa sababu timu yeyote inayotaka kujiimarisha lazima iwe na wachezaji wa kaliba ya Niyonzima hata zaidi ya mmoja ili kutorubusu kuwa tegemezi wa huduma ya mchezaji fulani na siku amekosekana timu inatetereka
 
Simba hawakuwa na shida ya kusajili kiungo msimu huu! Walikuwa na viungo bora kabisa kama Mo Ibrahim, Mzamiru, Ndemla! Mkude, Majavi, Kotei n.k! Sijui kwanini waliamua kutumia hela nyingi kumsajili Haruna ambaye hana alichowazidi hao niliowataja!
 
Unatudanganya wewe ni mshabiki was yanga unania tu ya kumchafua Niyonzima, hivi kunamchezaji simba wa kumlinganisha na niyonzima huyo simba imelamba Dume acha utani
Kupenda kusimfanye mwanadam akawa mtumwa wa fikra au Kipofu.Yeye ametoa mawazo yake na huo ndio ukweli mchungu ambao inabidi muukubali
 
Kupenda kusimfanye mwanadam akawa mtumwa wa fikra au Kipofu.Yeye ametoa mawazo yake na huo ndio ukweli mchungu ambao inabidi muukubali
Hoja yako ni nzuri sema unaonesha ww ni wa upande wa pili, hebu tizama clubs kubwa za wenzetu ulaya zilivyo na wachezaji wazuri tena kwenye eneo moja! Hili si kosa boss
 
Tatizo wanamchezesha kwenye wings instead ya center. Angalia cross zake uchwara
 
Harumoney.
Kama Ngasa atarudi Yanga mwishowe
 
wewe acha kumfananisha POGBA na vitu vya kijinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…