Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kutokana na umri kusogea sana imenibidi nipunguze mambo ya starehe kama; kwenda sehemu za starehe, kunywa pombe, kucheza na warembo pamoja na kuchepuka.
Nimeamua kujituliza ili niwaachie na wengine waweze kujiburudisha kwenye hayo mazingira ya kujimwambafai.
Sasa changamoto iko hivi, wale walionizoea viwanjani na michepuko wamekuwa wakinipigia simu na kuniuliza, ''mbona uonekani kwenye viwanja?''
Nami nawajibu, ''uzee umenisogelea najaribu kwa sasa kuweka akiba ya uzeeni na ya kwenda kuishi huko kijijini; kwa sababu maisha ya mjini yameshanichosha.''
Wanakata simu kwa hasira na kuniita, ''wewe bwege nini, wakati tulipokuwa tunakunywa na kutupelekea moto vizuri hukujua hayo?''
Nabakia tu kucheka; kwa sasa nikiwapigia simu, hawapokei simu zangu, nimekuwa kama simba dume mzee niliye telekezwa.