Baada ya kuashiria kuingia Israel, Erdogan apiga hatua moja zaidi. Amwambia Biden uchokozi wa Israel utasababisha moto kusambaa kote Mashariki ya Kati

Baada ya kuashiria kuingia Israel, Erdogan apiga hatua moja zaidi. Amwambia Biden uchokozi wa Israel utasababisha moto kusambaa kote Mashariki ya Kati

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kufuatia kuuliwa kwa kiongozi mkuu wa Hamas hapo juzi,raisi Erdogan wa Uturuki amempigia simu raisi Biden na kutoa onyo kwa kusema kama ifuatavyo na kama ilivyoripotiwa na Aljazeera

Turkey’s leader Recep Tayyip Erdogan in a phone call with US President Joe Biden says Israel’s killing of Hamas leader Ismail Haniyeh “dealt heavy blow to ceasefire” talks, shows Netanyahu government wants “fire in Gaza” to spread regionally.

Tamko lake hilo linafuatiwa na kauli yake ya wiki iliyopita baada ya kuona uonevu dhidi ya Palestina umepitiliza mipaka aliposema kuwa nchi yake itaingia Israel ili kuwasaidia wapalestina.

Kama mfuatiliaji wa vita hivi kwa muda mrefu tangu juzi nywele zimekuwa zikinisisimka na uzoefu wangu kuna kitu kikubwa kitatokea hapo Israel na mashariki ya kati muda si mrefu kutokana na vita hivi.

Kwa vile hukumu za mahakama na maazimio ya umoja wa mataifa yameshindwa kuizuia Israel kufanya mauwaji mabaya kwa wapalestina vikao hivyo havitokuwa na wa kuvisikiliza tena.
 
Vita haiepukiki hapa middle East, huku waarabu wanatafuta amani wakiwe wameficha mapanga nyuma, Iran alishamwambia Israel kubwa amezungukwa pande zetu na wapiganaji wetu, na akasema ataifuta Israel kwenye ramani ya dunia. Kwa mazingira hayo Israel akilegeza kamba ameisha, wanadai wayahudi warudi Ulaya ili palestinians wabaki na nchi yao.
 
YESU ATUSAIDIE UGOMVI SIO KITU KIZURI DAIMA IWE KWA ANAE PIGA AU ANAE PIGWA.
 
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdowan (Erdogan) amedai Israel inafanya maksudi kwa kuwaua viongozi wa Hezbollah Hamas na Iran ili vita itoke ukanda mzima wa mashariki ya kati. Lakini wameshawashtukizia watadeal nao siku inakuja.

========

Turkey’s leader Recep Tayyip Erdogan in a phone call with US President Joe Biden says Israel’s killing of Hamas leader Ismail Haniyeh “dealt heavy blow to ceasefire” talks, shows Netanyahu government wants “fire in Gaza” to spread regionally.

Source: Al Jazeera

20240802_090953.jpg
 
Vita haiepukiki hapa middle East, huku waarabu wanatafuta amani wakiwe wameficha mapanga nyuma, Iran alishamwambia Israel kubwa amezungukwa pande zetu na wapiganaji wetu, na akasema ataifuta Israel kwenye ramani ya dunia. Kwa mazingira hayo Israel akilegeza kamba ameisha, wanadai wayahudi warudi Ulaya ili palestinians wabaki na nchi yao.
Netanyahu yeye hataki hata nafuu ya mataifa mawili aliyopewa na Arafat.Sasa atakosa yote au ataishi kwa wasi wasi mkubwa.Wananchi wa Israel hawana furaha tena kuishi kwenye majumba yao kama ilivyokuwa hapa awali
 
Huyu dalali siyo wa kumwamini.. Erdogan mda siyo mrefu ataondolewa madarakani na raia..
Mbinu hizo za kuondosha watu madarakani hazijafanikiwa isipokuwa kwa waarabu.Venezuela na kwengineko imeshindikana kabisa.
 
Back
Top Bottom