Baada ya kueleza hatimaye leo Taa za barabara eneo la CUoM Mbeya zinarekebishwa, hongereni TANROADS

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079

Jana niliandika kuhusu changamoto ya taa za kuongozea magari na watembea kwa miguu zilizopo eneo la Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mbeya (Catholic University of Mbeya - CUoM), ambazo zilikuwa hazifanyi kazi kwa takribani wiki moja licha ya kuwa bado ni mpya baada ya kufungwa Mei 2026.

Soma DOKEZO - Taa za Kidigitali zilizozinduliwa Mei 2026 na TANROADS eneo la Chuo cha CUoM - Mbeya, zina wiki hazifanyi kazi

Awali, ilielezwa kuwa taa hizo ni za kidigitali na zilitarajiwa kuongeza usalama kwa madereva pamoja na watembea kwa miguu wanaotumia eneo hilo.

Leo Julai 28, 2026, baada ya kupita mitaa hiyo, tumekuta mafundi wakiwa katika eneo hilo wakifanya marekebisho ya taa hizo.

Hatua hiyo ni jambo jema na inaonesha mwitikio wa mamlaka husika katika kushughulikia changamoto za miundombinu ya umma. Nawapongeza TANROADS kwa kuchukua hatua na kuendelea kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara unarejea katika hali nzuri.
 
Why moaka wasukumwe, walalamikiwe?
 
angalau hata hawa wamechukua hatua sio taasisi zingine ni ujinga mtupu unalalamika miaka 2 hakuna jambo wanabadirisha
 
Back
Top Bottom